M/KITI WA UVCCM KILIMANJARO ALIYEHAMIA CHADEMA, ARUDI CCM - KUONGEA NA WAANDISHI LEOPARD HOTEL, MOSHI.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Kilimanjaro ndugu Fredrick Mushi ambaye wiki moja iliyopita alijiunga na CHADEMA akitokea CCM na kupokelewa na wajumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, ameandika barua kwa Katibu Mkuu wa UVCCM ndg Sixtus Mapunda akiomba kurudishwa kwenye nafasi yake hiyo ya awali.
Katika barua yake, Ndugu Mushi ameueleza uongozi wa juu wa UVCCM kuwa alijiunga na CHADEMA baada ya kuhadaika alipofuatwa na Viongoxi wa juu wa CCM waliokuwa wakimuunga mkono LOWASA pamoja na Mzee Ndesamburo na kumuambia kuwa wahame pamoja nae na kwamba atapatiwa milioni 20.
Na alipokamilisha zoezi la kuita waandishi wa habari na kujitangaza kuhama amekuwa akipigwa danadana kuhusu malipo yake na kwamba mpaka sasa hajapatiwa kiasi hicho cha fedha.
Mushi ambaye alikuwa ni miongoni mwa Vijana wanaomuunga mkono LOWASSA tangu akiwa CCM amesema amejaribu kumtafuta Mzee Lowassa mara kadhaa lakini bila mafanikio. Kwani simu zake kwa sasa zinapokelewa na wasaidizi na wanamjibu Mzee yuko busy.
Mushi ameomba kurudishwa katika nafasi yake kama Mwenyekiti wa Vijana UVCCM Mkoa wa Kilimanjaro na ameahidi kwa namna ile ile ya kuzungumza na waandishi wa habari, ataita tena waandishi wa habari kesho saa nne asubuhi, Leopard Hotel, Moshi mjini na kuongeza kuwa atazunguka kwenye majukwaa katika Mkoa wa Kilimanjaro na Arusha kuelezea uongo na ulaghai wa CHADEMA wakitumia fedha kuwahonga na kuwadanganya Vijana.
No comments:
Post a Comment