Huko kwenye kurasa za Jamii Forum kumekua na mjadala motomoto wa kisia uliohusisha wadau mbali mbali wa kisiasa na wanaharakati mbalimbali nchini. Hebu kuwa nasi ili kujua kilichojiri.
Kesho Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) kwa kushirikiana na moja ya wafadhili wa mtandao huo Open Society Initiative for Eastern Africa (OSIEA). utaendesha mkutano katika Hoteli ya Kilimanjaro ya Jijini Dar es Salaam mafunzo yatakayowakutanisha Tume ya Haki za Bindamu na Utawala Bora nchini, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Ernest Mangu, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Dk. Edward Hosea, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva, Jaji Mkuu wa Mahakaam Kuu ya Tanzania na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Fransis Mutungi,
Washiriki wengine ni pamoja na Onesmo Olengurumwa, Mratibu wa Mtandao wa (THRDC), Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda, Katibu Mkuu wa CCM, Nape Nauye, Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, Katibu wa Chama cha Wananchi (CUF) BAKWATA, Dr. Benson Banna (TEMCO), Peter Kuga Mziray- Mwenyekiti wa Chama cha APPT Maendeleo, Baraza la Maaskofu Tanzania(TEC) ,Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Chama Cha ACT Wazalendo na Chama Cha NCCR-Mageuzi wamethibitisha kushiriki mafunzo hayo.
Aidha, pamoja na mambo mengine watajadili mada juu ya dhana ya usalama katika kupindi cha uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka 2010 ikiwa ni pamoja na kuangalia suala la usalama kuwa lilizingatiwa kiasi gani, pamoja na kuangalia changamoto za uchaguzi huo ili kwa pamoja waweze kujadiliana kwa pamoja changamoto zinazoweza kujitokeza/kuepukwa zinazoweza kuchochea ghasia kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Octoba, 25, 2015.
============================== ==
Updates: 26 Aug 2015
Kinachojiri katika Hoteli ya Hyatt Regency leo
J. Jesse: kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, amesema vikundi vya Usalama vya vyama vinafanya hadi kazi ya kukamata, kuhoji na kuadhibu watu. Ni tishio la Usalama wakati huu
Amesema baadhi ya vyama vilivyohojiwa vilidai havina imani na Jeshi la Polisi, uwepo wa vikundi hivi ni kinyume na Katiba.
Kwa sasa anazungumza Salum Mwalimu (CHADEMA), anasema suala la Vikundi vya Vyama na Suala la Ulinzi & Usalama ni nyeti. Tunataka uchaguzi ufanyike kwa amani tushike Dola. Suala la Vikundi vya Usalama ktk Vyama bado linazungumziwa kisiasa. Utafiti uko wapi.
Anasema vikundi vya Usalama vya Vyama ni muhimu kwa Usalama wa Viongozi wetu. Mipaka ya Ulinzi wa Viongozi ipoje?.
Amesema wanaodai vikundi vya usalama vya Vyama vinapata mafunzo Kijeshi waseme mafunzo yanafanyika wapi?yeyote anayevunja Sheria akamatwe na ashughulikiwe. Vikundi hivi vipo kwa mujibu wa Katiba za Vyama.
Mwakilishi CUF: Vikundi vya Ulinzi vya Vyama vilikuwepo tangu zamani; tulikuwa wapi? Hakuna sehemu Katiba inazuia, Katiba za Vyama vyetu zilipishwa na Tume ya Uchaguzi na zinaainisha Uwepo wa Vikundi vya Usalama ktk Vyama.
Mwanaisha(ADC): Kama Vyama vya Siasa haviruhusiwi kuruhusiwi kuwa na Vikundi vya Usalama, kwanini Katiba za Vyama zilipitishwa?Kama Vikundi vya Vyama vinaruhusiwa, basi viwe na utambulisho kama ambavyo Polisi wanatambulika.

Salum Mwalimu (CHADEMA): Suala la Vikundi vya Vyama na Suala la Ulinzi & Usalama ni nyeti. Tunataka uchaguzi ufanyike kwa amani tushike Dola
Salum Mwalimu(CHADEMA): Suala la Vikundi vya Usalama ktk Vyama bado linazungumziwa kisiasa. Utafiti uko wapi?
Salum Mwalimu(CHADEMA): Vikundi vya Usalama vya Vyama ni muhimu kwa Usalama wa Viongozi wetu. Mipaka ya Ulinzi wa Viongozi ipoje?
Salum Mwalimu(CHADEMA): Wanaodai Vikundi vya Usalama vya Vyama vinapata mafunzo Kijeshi waseme mafunzo yanafanyika wapi
Salum Mwalimu(CHADEMA): Yeyote anayevunja Sheria akamatwe na ashughulikiwe. Vikundi hivi vipo kwa mujibu wa Katiba za Vyama
Jaji Mutungi (Political Parties Registrar): Wakati vyama Vinaanzishwa hali kisiasa haikuwa kama leo
Jaji Mutungi: Tusilaumiane kuhusu hili la Vikundi vya Ulinzi vya Vyama, tujadili hili tunalitatua vipi sasa kama wadau
Dr. Bana(TEMCO):
Tutafanya utafiti kuhusu Michakato ya Uchaguzi ndani ya Vyama. Tutachunguza kampeni zilivyofanywa
Dr. Bana(TEMCO):
Sisi tutafanya kazi kwa maslahi ya Taifa. We will be impartial
Jaji Mkwawa (from NEC): Tunasisitiza, ni muhimu watu kwenda kuhakiki majina yao kwenye Daftari la Wapiga Kura
Jaji Mkwawa(NEC): Matumizi ya lugha zinazoweza kupelekea uvunjaji wa Amani yaepukwe. Maadili ya Uchaguzi yazingatiwe
Jaji Mkwawa(NEC): Hatutarajii Vyombo vya Dola kufanya vitendo vinavyoweza kuwaogofya watu kwenda kupiga kura
Jaji Mkwawa(NEC):
Jaji Mkwawa(NEC): Hatutarajii Vyombo vya Dola kufanya vitendo vinavyoweza kuwaogofya watu kwenda kupiga kura
Jaji Mkwawa(NEC):
Mimi mwenyewe sifahamu kama kuna sheria ya kuzuia kubandika Matokeo ya Urais vituo vya Kupigia Kura
Jaji Mkwawa(NEC):
Sisi kama Tume tutajitahidi kujenga imani kwa wananchi. Sisi ni Tume Huru wala hatupokei maelekezo toka kokote
Chagonja (TZ Police): Kuna haja ya kuandaa taratibu na kanuni za uendeshaji wa Vikundi vya Ulinzi ktk Vyama vya Siasa
Chagonja(TZ Police): Idadi ya Polisi TZ haizidi 45,000. Jukumu la Ulinzi na Usalama lipo zaidi mikononi mwa wananchi
Chagonja(TZ Police):
Vikundi vya Ulinzi ktk Vyama vya Siasa havitakiwi kuchukua majukumu ya Jeshi la Polisi
Chagonja(TZ Police):
Polisi hatuna upande kuegemea ktk Uchaguzi. Tutatimiza wajibu na kusimamia sheria
Chagonja(TZ Police):
Zinatakiwa kuchukuliwa hatua za haraka kuweka mipaka ya Vikundi vya Usalama vya Vyama vya Siasa
Mary Mosha(PCCB):
Sisi TAKUKURU tumepokea malalamiko ya Rushwa katika michakato ya Uchaguzi katika Vyama na wengine tumewakamata
Jaji Mutungi(Msajili wa Vyama):
Tusiwe wanyonge! Kuna Mataifa yanashangaa tumefika hatua hii bila kukwaruzana! Hatuigizi
Jaji Mutungi(Msajili wa Vyama):
Vyama vyote vya Siasa vilitakiwa kuwa vimewasilisha Timu za walio kwenye Kampeni za Urais
Jaji Mutungi:
Ni chama 1 tu kilicholeta taarifa ya watakaokuwa kwenye timu ya kampeni ya mgombea urais. Sheria zipo
Jaji Mutungi:
Wakati tukiwataka Polisi na Vyombo vya Dola vitende HAKI, nasi tujitahidi kutekeleza WAJIBU wetu
Jaji Mutungi:
Sheria zipo, lakini Dhamira ndiyo iwe msingi mkubwa ktk kuhakikisha tunakuwa na Uchaguzi wa Haki na Amani
Machumbana(Jukwaa la Katiba):
Tume ya Uchaguzi ni ya wateule wa Rais ambaye ni Mwenyekiti wa CCM, siwezi kusema ni Huru
Muhanika(MOAT):
Ufanyike utaratibu Jeshi la Polisi likae na Vyama vya Siasa kuangalia jinsi ya kutatua hili la Vikundi vya Ulinzi
Sheikh Mkuu Dar: Mwaka 2010 Viongozi wa Dini tuliwatembelea wagombea wote, naomba 2015 tufanye hivi tena kuhubiri amani
Sheikh Mkuu Dar: Ni muhimu HAKI, UTII WA SHERIA, UHURU WA KUCHAGUA vikazingatiwa kwa wadau wote wakati huu
Salum Mwalimu(CHADEMA): Nawashukuru NEC kuthibitisha kuwa Matokeo ya Urais yanatakiwa kubandikwa vituoni
Salum Mwalimu(CHADEMA): Tukae tuzungumze na Jeshi la Polisi jinsi ya kuvisimamia Vikundi vya Ulinzi vya Vyama. Hii itasaidia
Salum Mwalimu(CHADEMA): Ni vema vikaitishwa vikao, matamko ya awali dhidi ya Vikundi vya Ulinzi vya Vyama yasitishwe tupate suluhu
Salum Mwalimu(CHADEMA): Tumetukanwa hivi majuzi, NEC wala Msajili wa Vyama hawakutokeza, tutajibu mapigo mwendelee kuwa kimya
Dr. Pindi Chana(CCM): Je, tunaweza kuwa na mstari wa wanawake hasa wajawazito na wenye vichanga?
Chagonja: Nawashauri UKAWA wasilipize Matusi waliyorushiwa, wajikite katika "issues", wenye akili wataelewa na kuamua
Ramadhani Mapuri(NEC): Kama umeenda ukakuta jina lako halipo/limekosewa ni vema ukatoa taarifa ili marekebisho yafanywe
Ramadhani Mapuri(NEC): Kama ulijiandikisha kwingine na sasa umehama, wahi sasa ukafanye marekebisho hayo mapema
R. Mapuri(NEC): Utaandaliwa utaratibu mzuri kwa akina mama wajawazito & wenye vichanga washiriki Uchaguzi Oktoba 25
R. Mapuri(NEC/ZEC): Suala la Vikundi vya Ulinzi vya Vyama linahitaji suluhu ya haraka na tutalifanyia kazi na wadau wote

No comments:
Post a Comment