
Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Nd. Nape Nnauye akizungumza na
waandishi wa habari nje ya ukumbi wa White House, Makao Makuu ya Chama Cha
Mapinduzi mjini Dodoma. Katika taarifa yake amethibitisha taarifa zilizotawala
vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuhusiana na mijina matano
yaliyoteuliwa na kikao cha Kamati Kuu ya CCM katika mchakato wa kumpata mgombea
urais katika uchaguzi mkuu kwa tiketi ya chama hicho chenye nguvu katika siasa
za Tanzania. Kwa mujibu wa Bw. Nape Nnauye, waliofuzu kuingia hatua ya tano
bora ni 1). Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe; 2) Waziri wa Ujenzi, Mh. John Mgufuli; 3) Waziri wa Katiba na
Sheria Mh. Asha-Rose Migiro, 4) Naibu Waziri wa
Mawasiliano, Mh. Januari Makamba, na 5). Balozi wa Kudumu wa Africa nchini Marekani, Mh. Amina Salum Ali
Majina
hayo ndio yamekua agenda kuu kujadiliwa katika kikao cha Halmashauri kuu ya CCM
ambapo maamuzi yataweka muafaka na kuwachuja kupata tatu bora ambayo
itawasilishwa katika kikao cha Mkutano Mkuu takaofanyika katika ukumbi mya wa
CCM mjini Dodoma na hatimaye kupatikana jina mija la ambaye atakuwa mgombea
Urais katika uchaguzi mkuu wa mwezi
October mwaka huu.
No comments:
Post a Comment