

HALI SI SHWARI NDANI YA KIKAO NCHIMBI AJA JUU ASEMA HAWAKUBALIANI NA MAAMUZI YA KUMUENGUA LOWASA..ASEMA YEYE, KIMBISA NA SOPHIA SIMBA WATAKWENDA KUWAMBIA WAJUMBE WAO KWAMBA HAWATAKUBALIANA NA MAAMUZI YA KIKAO HICHO KWANI KINA MALENGO Y KUMKATAA MTU ANAYE PENDWA NA WENGI BILA YA SABABU YEYOTE NA KUWALETEA MAJINA MATATU WALIYO KWISHA YACHUKUA WAO..HATA HIVYO ALIGOMA KUYATAJA MAJINA HAYO AKISEMA HAYO MAJINA YATATAJWA NA NAPE AMBAYE NDIYE MSEMAJI WA CCM.

Wametoka na kutoa tamko kwamba hawakubaliani na maamuzi ya wajumbe wenzao.
Wanasema majina waliyoletewa ni baadhi tu.
Hawajataka kuzungumza zaidi
Hata hivyo Dr. Nchimbi alionekana ni mwenye jazba kubwa jambo linalodhihirisha kuwa alikuwa na mgombea wake, ambaye hakupitishwa na Kikao cha Kamati Kuu kuingia 5 bora. Kutokana na ratiba ilivyo, kikao cha Halmashauri kuu na Mkutano Mkuu wa CCM kuanza kufanyika asubuhi hii, jambo linaloweka ugumu wagombea wasioridhika na maauzi hayo kukata rufaa na kuzingatiwa katika vikao hivyo vya juu vya maamuzi.
Tazama video hapa >>>>>>>>>>>>>>>
No comments:
Post a Comment