Saturday, July 11, 2015

WAFAHAMU WATANO BORA CCM


Mfahamu Bernard Kamilius Membe, mmoja wa wagombea watano.
Ni mbunge wa jimbo la Mtama (2000 - 2015), na waziri wa mambo ya nje Tanzania (2007-2015). Mhe. Membe amesomea Sayansi ya Siasa katika Chuo Kikuu Cha Dar-es-salaam na Mahusiano ya Kimataifa katika chuo cha Johns Hopkins, na amepitia mafunzo ya kijeshi (nationa service) kwa mwaka mmoja katika kambi la kijeshi la Oljoro (Arusha)


Mfahamu John Pombe Magufuli, mmoja wa wagombea watano.
Ni mbunge wa jimbo la Biharamulo Mashariki Tanzania, na ni waziri wa ujenzi (2010-2015). Amesomea shahada ya uzamivu ya Kemia katika chuo kikuu cha Dar-es-salaam.


Mfahamu Asha-Rose Migiro, mmoja wa wagombea watano. 
Ni Mbunge wa kuteuliwa katika bunge, na waziri wa sheria na katiba Tanzania. Mhe. Migiro amesomea sheria katika Chuo Kikuu Cha Dar-es-salaam na shahada ya uzamivu yake katika chuo cha Konstanz (Ujerumani). Kabla ya kujiunga na siasa, alikua mhadhiri mkuu wa mafunzo ya sheria Chuo Kikuu Cha Dar-es-salaam. Pia aliwahi kuwa naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa (2007-2012)


Mfahamu January Makamba, mmoja wa wagombea watano. 
Ni Mbunge wa Bumbuli (2010-2015), na naibu waziri wa mawasiliano, sayansi, na teknolojia Tanzania (2012-2015). Amesomea shahada ya uzamivu katika diplomasia na usuluhishi wa migogoro katika chuo cha George Mason, kabla ya kuwa msaidizi wa Rais Jakaya Kikwete


Mfahamu Amina Salum Ali, mmoja wa wagombea watano.
Aliwahi kuwa waziri wa Fedha (Zanzibar; 1990-2000), na ni balozi wa Umoja wa Mataifa ya Afrika nchini Marekani (2007-2015). Amesomea uchumi katika chuo cha Delhi na pia ana MBA ya Masoko kutoka chuo cha Pune.

No comments:

Post a Comment