TIMU YA AZAM YADHIHIRISHA UBABE KOMBE LA KAGAME. YATINGA NUSU FAINALI
Klabu ya Azam FC imezidi kufanya vizuri katika
michuano ya Kombe la Kagame ambalo linaendelea Dar es Salaam...Azam FC amabayo ilianza kufanya vizuri katika
mashindano hayo toka mechi ya kwanza kwa kuifunga KCC ya Uganda kwa goli 1-0, goli pekee ambalo
lilifungwa na John Bocco dakika ya 9 ya mchezo.
July 25 Azam
FC imetinga
Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kucheza mchezo wake wa mwisho wa
kundi C dhidi ya Adama City ya Ethiopia… Azam
FC imeifunga Adama Cityya Ethiopia kwa jumla ya magoli 5-0 magoli amabyo
yamepachikwa wavuni na Kipre Tchetche dakika ya 7 na 19, Farid Mussa dakika 31, Mudathir Yahya dakika ya 49 naAggrey Morris dakika ya 73 kwa mkwaju wa penati.
Kwa matokeo hayo Azam
FC inaongoza
kundi C kwa jumla ya point 9 nyuma ya KCC FCya Uganda ambayo ipo nafasi ya pili huku nafasi
ya tatu ikishikwa na Malakia ya Sudani Kusini na Adama City ya Ethiopia ikishika mkia, sasa Azam FC itacheza Robo fainali na mshindi wa pili wa kundi A.
No comments:
Post a Comment