MH. N'HUNGA ATOA MSAADA WA VIFAA VYA UJENZI KITUO CHA AFYA CHA MASINGINI
Mh. Mihayo N'hunga akisaini kitabu cha wageni alipowasili Kituoni hapo.
Mwakilishi wa Jimbo la Mwera Mh. Mihayo N'hunga na Mwenyinti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Magharibi mjini Ungujan-Zanzibar, leo amekabidhi vifaa mabali mbali vya ujezi katika zahanati (Kituo cha Afya) cha Masingini ili kufanikisha kukamilisha ukarabati wa kituo hicho cha afya ambacho kilifikia kusimamisha kutoa huduma kufuatia kuwa na miundombinu mibovu na chakavu. Katika tukio hilo vifaa pamoja na Saruji, Matofali, Mchanga, Ndoo za rangi, Kokoto, Nyavu za Madirishani, Magodoro pamoja na vingine vingi vya ujenzi na vya matumizi mengine kwa Uongozi wa Kituo hicho cha afya kilichopo Masingini.
Akiwasilisha mchango huo wenye thamani ya zaidi ya Shilling Million tatu, ikiwa ni sehemu ya kutekeleza ahadi zake kwa wananchi wa jimbo la Mwera, Mh. Mihayo pia alishauri kuhakikisha vifaa hivyo vinatumika kwa malengo stahiki ili kufanikisha ukarabati wa kituo hicho cha afya haraka. "Vitu hivi, visitumiwe kwa malengo mengine nje ya nje ya Zahanati hii, ili tuweze kuona huduma za afya zinarejea haraka na wananchi wanufaike vzuri" alisema Mwakilishi huyo.
Akizungumza baada ya kupokea mchango huo, Mkuu wa kambi ya Masingini amesema, anashukuru sana kwa mchango huo wa mwakilishi katika Kituo cha afya ambacho ni tegemeo kubwa sio tu na wanachi wakaazi wa Masingini tu, bali hata kwa askari wake, na kwamba atasimamia kuona vifaa hivyo vitatumika vizuri na atafurahi kuona huduma za afya zinarejea kitukni hapo.
Mh. Mihayo N'hunga ni miongoni mwa wawakilishi wenye umri mdogo zaidi waliochaguliwa na wananchi majimboni, wananchi wa jimbo la Mwera wana matumaini makubwa kwake kutokana na jitihada zake kuhakikisha anahamasisha maendeleo kwa kasi. Hivi karibuni mwakilishi huyo alichaguliwa na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa NEC.
Mh. Mihayo N'hunga akiwa kwenye picha ya pamoja na mke wa Mgunge wa Jimbo hilo Bi. Asha pamoja na askari wa KMKM
No comments:
Post a Comment