
Baada ya kusiliza na Kupitia hotuba za wagombea kwa makini, nimegundua kua Mh. Balozi Amina Salum Ali amewasilisha hotuba yenye mashiko zaidi ya wagombea wenzake, kisha Mh. John Magufuli na ikifuatiwa na ile ya Mh. Asha-Rise Migiro. Tunaamini wazi kuwa uzuri wa hotuba ya mgombea sio kigezo cha alama ua ushindi bali ni wingi wa kura ndio humaliza mchakato wa uchaguzi. Balozi huyu anategemea kupata kura nyingi miongoni mwa wajumbe kutoka Zanzibar, wajumbe wanawake, na miongoni mwa wajumbe wanaomuunga mkono Mh. Edward Lowasa (Hili limedhihirika katika hotuba yake wakati akiomba kura)
Mh. John Magufuli ameonekana ni mgombea mwenye mvuto zaidi kwa wajumbe wa mkutano mkuu na hata kwa sehemu kubwa ya nchi yetu tangia mara tu baada ya kufuzu kuingia fainali (3 bora). Taifa zima linategemea Magufuli kuibuka mshindi katika mchakato huu na hatimaye kuwa mgombea mteule wa Urais CCM katika uchaguzi mkuu. Magufuli anategemewa kupata kura nyingi miongoni mwa wajumbe wa hasa Tanzania Bara, na zaidi ukanda wenye wajumbe wengi (Kanda ya Ziwa) na zaidi wajumbe wasiopenda kuongozwa na wanawake.
Mh. Asha-Rose Migiro ni mgombea mwenye haiba kubwa katika siasa za nchi yetu, na ni mwenye uzoefu wa kipekee kTika utumishi wa umma ndani na nje ya nchi yetu, hata hivyo hakuweza kupangilia vyema hotuba yake ya kuomba kura kama wengi tulivyo tarajia. Ni mgombea mwenye mvuto zaidi hasa ukilinganisha na wagombea wengine wote, hata hivyo anategemewa kupata kura nyingi miongoni mwa wajumbe wanawake, vyuo vikuu, na watumishi wa serikali pia.
TATHMINI
Inaonekana kuwapo uwezekano mkubwa mshindi wa mchakato akawa ni Mwanamke na kura nyingi kumchagua Balozi Amina Salum Ali.
1)Kama wajumbe toka Zanzibar watakuwa wamepiga kura kuelekea kwa mgombea anayetokea Zanzibar.
2) Kama wanawake wamepiga kura zao kwa wagombea wa kike
3) Kama wajumbe wa kundi la Lowasa watampigia (Imeonekana ktk hotuba yake kana kwamba kuna mpango wa kuhamisha kura za Lowasa kwa Balozi Amina).
Binafsi nilim-beza Balozi Amina siku aliyo chukua fomu ya kuwania nafasi hiyo, Bali niamini angeweza kufuzu 5 bora na safari yake ingeishia hapo. Lakini mpak sasa inaonekana kama mshindi atapita kwa kishindo basi atakua Balozi Amina, wakati nikiamini Mh. Migiro ataibuka na ushindi nafasi yatatu.
No comments:
Post a Comment