Sunday, September 20, 2015

MIHAYO N'HUNGA AANZA KUNADI SERA BAADA YA KUZINDUA RASMI KAMPENI ZAKE KUWANIA UWAKILISHI



Chama Cha Mapinduzi (CCM) jimbo la Mwera kisiwani Unguja (Zanzibar) kimezindua rasmi kampeni zake ngazi ya jimbo kwa wagombea ngazi za Ubunge, Udiwani na Uwakilishi, ambapo umati mkubwa wa wanachama jimboni hapo walijitokeza ili kusikiliza sera za wagombea hao.
Mgombea Uwakilishi kupitia CCM jimboni hapo Bw. Mihayo N'hunga ambaye katika uzinduzi huo wa kampeni jimboni hapo ambaye ameongozana na makada mbalimbali wakiwemo Mgombea Ubunge wa jimbo hilo Bw. Makame Khamis, Diwani wa wadi ya Mwera Bi Sham ambaye pia ni mgombea wa nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu kupitia CCM.
Mwenye kiti wa Jumuiya ya wazazi ya CCM mkoa wa Mbeya Bi Fatuma Kasenga  ndiyo alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo ya uzinduzi wa kampeni hizo ambapo katika hotuba yake amehimiza kwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kuendelea kuwa wavumilivu licha ya propaganda na siasa za maji taka kutoka kwa wapinzani wao kisiasa. Akihutubia maelfu ya waliojitokeza katika uzinduzi huo, Bi Fatma Kasanga amesema, "Ndugu wana CCM, mwaka huu uchaguzi unaonekana kuwa na hamasa kubwa na wapinzani wanatumia propaganda, matusi na kejeli; lakini ndugu zangu tuwe wavumilivu sana na siasa zao za majitaka". Mgeni rasmi pia baada ya kuwatambulisha aliwanadi na kuwaombea kura wagombea wa CCM jimboni hapo na kuwataka washirikiane kuhakikisha CCM inapata ushindi mkubwa wa pamoja ili waweze kupata fursa nzuri kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo la Mwera.Naye mgombea Uwakilishi Bw. Mihayo N'hunga amesisitiza kuhakikisha kuleta maendeleo ya kiuchumi hasa kwa vijana ambao wengi wao ndio nguvu kazi kwa maendeleo ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla. Ameeleza kuwa atashirikiana vyema na m-bunge pamoja na madiwani kuwapigania vijana kwa kengo la kuwakwamua kiuchumi akiamini kwamba vijana ndio rika kubwa linalogusa kila familia na akasisitiza kwamba kumkwamua kijana ni kuijenga Zanzibar na Tanzania nzima.Akijibu hoja zinazoenezwa na wapinzani wake Bw. Mihayo amesema kwamba wanaodai kuwa yeye ni mdogo na hawezi kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo, je wao waliwatendea nini wananchi hao enzi za ujana wao. Mihayo amesikika akisema " Kuna wanao sema kuwa eti mimi ni mdogo, waulizeni wakati wao wakiwa na umri kama wangu, waliwatendea nini wanajimbo na wananchi".Alimalizia hotuba yake kwa kuwahakikishia wanachama wa chama hicho cha CCM kuwa waondoe shaka kwani safu nzima ya wagombea wa CCM jimboni hapo ni vijana wachapa kazi tu na kwamba wapo tayari kusimamia vyema ilani ya chama cha Mapinduzi kwani imesheheni mahitaji yote ya msingi. 

Kuelekea uchaguzi mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika October 25 wa uchagua viongozi wa ngazi za Rais, Ubunge, Uwakilishi (Zanzibar) na Udiwani, kwa jimbo la mwera Chama cha Mapinduzi (CCM) kinawakilishwa na wagombea mahiri ambao ni Bw. Makame Khamis (Ubunge), Bw. Mihayo N'hunga (Uwakilishi), na madiwani wawili ambao ni Bi Shani O. Mbena (Wadi ya Mwera) na Bw. Suleiman Abbas (Wadi ya Kianga). Kampeni hizo zilizinduliwa rasmi siku ya Ijumaa tarehe 18/09/2015 katika viwanja vya Misufini na kufuatiwa na mkutano wa hadhara kwa ajili hiyo uliofanyika Regeza Mwendo katika viwanja vya afisi za wilaya ya Magharibi nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

              Bw. Mihayo N'hunga akiwa kwenye picha ya pamoja na Bi Khadija Mussa Bi Amina muda mfupi kabla ya mkutano wa hadhara
 


No comments:

Post a Comment