Wednesday, August 19, 2015

SHIGONGO AWEKA WAZI UMAHIRI WA MAGUFULI KIMAENDELEO


Soma hapa alichoandika Eric Shigongo katika ukurasa wake wa facebook. 
Ningeweza kutumia maneno mengi sana kama mgombea urais aliyechaguliwa a Chama Cha MApinduzi (CCM), John Pombe Magufuli asingekuwa mchapakazi. Ningekutumia zaidi ya maneno laki moja kuzungumzia chochote kile alichokifanya endapo tu Magufuli asingefanya kile kitu alichoagizwa na Watanzania kukifanya.
Leo hii ninasimama kifua mbele na kujiamini kwamba mgombea huyu wa tiketi ya Chama cha Mapinduzi ni mchapakazi ambaye kila mmoja angetamani kuwa na mtu kama huyu.
Nani hafahamu utendaji wake kazi, nani hafahamu umakini aliokuwa nao katika utendaji kazi, uadilifu na uaminifu kiasi kwamba chama tawala cha CCM kimemwamini.
Watanzania wenzangu, wanaume kwa wanawake, warefu kwa wafupi, weupe kwa weusi, watu wa rika zote na rangi zote, huyu ndiye mtu pekee tuliyekuwa tukimuhitaji, mchapakazi ambaye atatutoa kimasomaso na kutufanya kusonga mbele.
Hii ni nafasi yetu pekee, nafasi ya kubadilisha historia ya nchi hii, nafasi pekee ya kusonga mbele kutoka pale tutakapoachwa na rais aliyeko madarakani, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete.
Kura yako moja kwa John Pombe Magufuli itayabadilisha maisha yako na kizazi chako. Nafasi ni yako.
MunguIbariki TAnzania.
Mungu ibariki CCM
Amen

No comments:

Post a Comment