Monday, August 17, 2015

N'HUNGA ACHUKUA FOMU RASMI KUWANIA UWAKILISHI JIMBO LA MWERA


MGOMBEA Uwakilishi jimbo la Mwera kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mihayo N’hunga ambaye aliongozana na Katibu wa UVCCM wilaya ya Mfenesini pamoja na Katibu wa CCM jimbo la Mwera na makada wengine mashuhuri jimboni hapo, leo amechukua fomu ya kuwania nafasi hiyo katika ofisi za Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC). 

Msafara wa Mihayo N’hunga ulifika katika ofisi za ZEC huku akisindikizwa na makada wa chama hicho jimbo la Mwera wakiwemo: Katibu wa CCM jimbo la Mwera, Katibu mwenezi wa Jimbo, Katibu wa wilaya UVCCM wilaya ya Mfenesini, Katibu Mwenezi.

Baada ya kuwasili katika ofisi hizo, mgombea huyo alitumia muda wa dakika kadhaa kukamilisha zoezi la kuchukua fomu kisha kurejea katika viwanja vya ofisi za CCM wilaya ya magharibu zilizopo Regeza Mwendo ambapo alikutana na wanachamba wa chama cha Mapinduzi waliojitokeza kumuunga mkono.

M/kiti wa UVCCM mkoa wa mjini magharibi na mgombea Uwakilishi CCM jimbo la mwera Mihayo N'hunga akionesha mkoba wenye fomu za kugombea uwakilishi, akiwa na kada mashuhuri wa CCM ndugu Suleiman Juma (Ticha Sele) mara baada ya kuchukua fomu ya kugombea uwakilishi katika uchaguzi mkuu october mwaka huu
M/kiti wa UVCCM mkoa wa mjini magharibi na mgombea Uwakilishi CCM jimbo la mwera Mihayo N'hunga akisaini kitabu maalum cha wagombea alipowasili katika ofisi za Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC kwa ajili ya uchukuaji fomu za kugombea Uwakilishi katika uchaguzi mkuu mwaka huu.


 M/kiti wa UVCCM mkoa wa mjini magharibi na mgombea Uwakilishi CCM jimbo la mwera Mihayo N'hunga akibadilishana fikra na Katibu wa UVCCM Wilaya ya Mfenefini muda mfupi kabla ya kuchukua fomu kuwania Uwakilishi.







 M/kiti wa UVCCM mkoa wa mjini magharibi na mgombea Uwakilishi CCM jimbo la mwera Mihayo N'hunga akikabidhiwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wilaya ya Magharibi Zanzibar mkoba wenye fomu za kugombea nafasi ya Uwakilishi jimbo la Mwera



 M/kiti wa UVCCM mkoa wa mjini magharibi na mgombea Uwakilishi CCM jimbo la mwera Mihayo N'hunga akiwa na baadhi ya makada waliojitokeza kumsindikiza zoezi la uchukuaji fomu kwa kijana wao. Kulia ni mjomba wa mgombea huyo bw. Mustafa Juma.







 M/kiti wa UVCCM mkoa wa mjini magharibi na mgombea Uwakilishi CCM jimbo la mwera Mihayo N'hunga akiwa na mwalimu wake wa siasa ambaye pia ni mjomba Ndugu Suleiman Juma.










No comments:

Post a Comment