Wednesday, August 5, 2015

MIHAYO N'HUNGA ASISITIZA KUFIKIA MALENGO YA AHADI ZAKE KWA WANAJIMBO KUZINGATIA ILANI YA CCM

MWAKILISHI MTEULE CCM ATOA SHUKRANI ZAKE KWA WANAJIMBO LA MWERA

Mkutano mkuu wa hadhara na wanachama wa CCM jimbo la mwera umefanyika jana, ambapo Mgombea huyo wa UWAKILISHI Bw. Mihayo N'hunga alitumia fursa hiyo kutoa shukrani zake kwa wanachama na wanajimbo wote kwa ujumla kwa ushindi waliompatia.


Katika shukrani zake amesema pia anawashukuru waliojitokeza kugombea nafasi hiyo pamoja naye ammo walikuwemo pia walimu wake, marafiki na wanachama wengine kwa ujasiri mkubwa, kwani mchakato ulikuwa mzito uliokuwa na changamoto nyingi. Hata hivyo amewapongeza kwa ujasiri mkubwa hasa walipo ridhia kukubaliana na matokeo ya uchaguzi huo wa kura za maoni.
N'hunga amesisitiza kua, katika mchakato wa kuomba kura kwa wana CCM amekua akitoa ahadi kadhaa kwa makundi mbalimbali, ikiwemo vijana, wanawake, wazee, na hata taasisi mbalimbali ambapo yeye alipata fursa ya kukutana nao wakati wa kampeni zake, kwamba atahakikisha anafikia malengo ya ahadi zake hizo endapo nitashinda uchaguzi mkuu kuwa Mwakilishi  kwani ahadi zote zinatekelezeka. 
"Hatijatoa ahadi ambazo hazitekelezeki kwenu, kwa sababu tuna dhamira ya dhati kuhamasisha maendeleo katika jimbo letu, muda umefika sasa nitahakikisha tunasimamia vema na tutafikia sehemu kubwa ya tuliyoahidi tena kwa muda mfupi, kwa sababu pia mambo yote yameelezwa katika ilani ya Chama chetu cha Mapinduzi CCM. Labda niseme wazi tu, nawaomba wagombea wenzangu tuliogombea mchakato wa kura za maoni, tujiunge pamoja kwani Tutashinda kwa Kishindo uchaguzi mkuu mwaka huu".  Alisema N'hunga.



Orodha ya wagombea UWAKILISHI CCM jimbo la mwera pamoja na kura walizopata katika uchaguzi wa kura za maoni zilizofanyika tarehe 01/08/2015 ambapo Bw. Mihayo N'hunga ameshinda kwa kura 321, akifuatiwa na Omar Gulam kura 184.

No comments:

Post a Comment