Tuesday, August 18, 2015

MEMBE, MAKAMBA, KINANA, NAPE, SOFIA SIMBA, SITTA, MWINGULU KUONGOZA KAMPENI CCM.

CCM YATAJA KAMATI YA KUMPELEKA MAGUFULI IKULU
Hawa ndio majemedari 32 wa ccm wataoshirikiana nasi wazalendo wa nchi hii katika kuinadi ilani na wagombea wa ccm ili kukipa chama ushindi wa kishindo
CCM YATEUA WAJUMBE 32 WA KAMATI YA KAMPENI
Chama cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania kimefanya uteuzi wajumbe 32 wa Kamati ya Kampeni kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu ili kuhakikisha inaibuka na ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi huo.
Akizungumza leo Jijini Dar es Salaama Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi CCM, Bw. Nape Nnauye amesema kamati hiyo itaongozwa na Katibu Mkuu wake Komredi Abdulrahman Kinana ambapo ameeleza kamati hiyo ni ya kuipatia ushindi CCM katika vinyang'anyiro vya udiwani, wabunge na urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.



No comments:

Post a Comment