Aliwahi
kuwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi Lawarence Masha amefikishwa katika
mahakama ya hakimu mkazi Kisutu Dar es salaam kwa kosa la kutumia lugha ya
matusi kinyume na sheria.
Baada
ya kutuhumiwa kuvunja kifungu cha sheria namba 89 kifungu kidogo 1,A cha mwaka
2002 cha makosa ya jinai, Lawarence Masha aliwasili majira ya 10:40 chini ya
ulinzi mkali.
Muda
wote tangu alipowasili mahakamani hapo mahakama ilikuwa chini ya ulinzi mkali
uliochagizwa na gari la maji ya washawasha.
Akisoma
shitaka mbele ya hakimu mkuu mkazi wa mahakama ya Kisutu Dar es Salaam
wariandere Lema, mwendesha mashitaka wa serikali Wankyo Simon ameiambia
mahakama kuwa mshitakiwa huyo Agast 24 katika kituo cha polisi cha Ostabay
alitumia lugha ya matusi ya wajinga nyie, washenzi hamna adabu na hamna dini
matusi yaliyokuwa yakimlenga askali Juma Mashaka na wenzake, shitaka ambalo
hata hivyo mtuhumiwa alikana na kutakiwa kuwa na wadhamini wawili waliopaswa
kusaini hati ya sh milioni moja kila mmoja ambapo suala la uhakikisha wa
wadhamini hao lilishindwa kukamilika kwa wakati na mtuhumiwa akalazika
kupelekwa gerezani Segerea.
Katika
hatua nyingine watuhumiwa zaidi ya 19 wanaodaiwa ni wa kundi M4U wamefikishwa
mahakamani hapo wakikabiliwa na mashitaki mawili yakiwemo ya kulanjama ya
kutenda kosa la jinai na kufanya mkusanyiko uliokuwa na nia ya kufanya
maandamano ambayo yangewafanya watu wa eneo la Moroko walipokuwa watuhumiwa hao
kuwa na fikra za uwepo wa uvunjifu wa amani.
Hata
hivyo kesi hiyo iliyokuwa ikisikilizwa na hakimu Emilius Mcharu huku
washitakiwa wakitetewa na wakili Peter Kibatala wamepelekewa Segerea baada ya
uhakiki wa dhamana zao kuchelewa kwa muda wote ambapo kesi hizo zilipokuwa
zikiunguruma mahakaamni hapo mahakaam ya Kisutu Dar es Salaam ilikuwa
imezungukwa na ulinzi mkali wa vikosi vya ulinzi na usalama.
No comments:
Post a Comment