KUELEKEA KURA ZA MAONI LEO HII MIHAYO N'HUNGA ANG'ARA JIMBO LA MWERA
Wakati mchakato wa kampeni ndani ya Chama Cha Mapinduzi CCM umekamilika, siku ya leo ndio iliyopangwa kwa ajili ya upigaji kura za maoni ili kupata mgombea atakaye peperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika October 25 mwaka huu 2015.
Mihayo N'hunga ni mmoja kati ya wagombea wanane (8) wanaowania nafasi ya uwakilishi kupitia Jimbo la Mwera, tathmini inaonesha kuwa N'hunga mpaka kufikia wakati huu, ameonekana kuungwa mkono na makada wengi mashuhuri na wenye nguvu ambao ni pamoja na Mh. Silvesta (Mbunge wa jimbo la Dole) ambaye ameshindwa kutetea nafasi yake ya Ubunge, ambapo Ndugu Makame Kassim Makame ameibuka kidedea mgombea ubunge jimbo la Mwera, pia aliyekuwa mwakilishi wa Jimbo hilo la mwera Mh. Shawana Buheti, na pia wajumbe wengi wa kamati ya siasa jimboni hapo. Umoja wa Vijana UVCCM jimboni hapo ndio ngome kubwa ambapo vijana wengi wameonesha kuvutiwa na sera za mgombea huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mjini Magharibi.
Endelea kuwa karibu blogu yetu tutawajulisha yanayojiri.
Hongera sana mkuu
ReplyDelete