Sunday, July 19, 2015

COCO BEACH DAR YAFURIKA EID PILI

KATIKA kusherehekea Sikukuu ya Idd Pili ambayo huadhimishwa na waumini wa Dini ya Kiislam duniani kote, leo wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wameonekana kufurika katika Ufukwe wa Coco Beach, uliopo Masaki jijini Dar, huku wengi wao wakijiachia kwa kuogelea na ‘kubarizi’ pembezoni mwa fukwe hizo.
Wengi waliojitokeza katika fukwe hizo ni watoto na vijana ambao muda wote walionekana wakiwa na furha.
Hapa ni baadhi ya picha zinazoonesha matukio ya wakazi hao wakiwa ndani ya bahari wakiogelea, huku wengine pembezoni.





No comments:

Post a Comment