Showing posts with label SPORTS. Show all posts
Showing posts with label SPORTS. Show all posts

Saturday, July 25, 2015

AZAM FC KUTINGA NUSU FAINALI KAGAME CUP

TIMU YA AZAM YADHIHIRISHA UBABE KOMBE LA KAGAME. YATINGA NUSU FAINALI



Klabu ya Azam FC imezidi kufanya vizuri katika michuano ya Kombe la Kagame ambalo linaendelea Dar es Salaam...Azam FC amabayo ilianza kufanya vizuri katika mashindano hayo toka mechi ya kwanza kwa kuifunga KCC ya Uganda kwa goli 1-0, goli pekee ambalo lilifungwa na John Bocco dakika ya 9 ya mchezo.
July 25 Azam FC imetinga Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kucheza mchezo wake wa mwisho wa kundi C dhidi ya Adama City ya Ethiopia… Azam FC imeifunga Adama Cityya Ethiopia kwa jumla ya magoli 5-0 magoli amabyo yamepachikwa wavuni na Kipre Tchetche dakika ya 7 na 19, Farid Mussa dakika 31, Mudathir Yahya dakika ya 49 naAggrey Morris dakika ya 73 kwa mkwaju wa penati.

Kwa matokeo hayo Azam FC inaongoza kundi C kwa jumla ya point 9 nyuma ya KCC FCya Uganda ambayo ipo nafasi ya pili huku nafasi ya tatu ikishikwa na Malakia ya Sudani Kusini na Adama City ya Ethiopia ikishika mkia, sasa  Azam FC itacheza Robo fainali na mshindi wa pili wa kundi A.

Friday, June 26, 2015

CLUB Y ASIMBA SPORT WAZINDUA TOVUTI YAKE



Afisa Mtendaji Mkuu wa EAG Group Imani Kajula Akimwelezea Jambo Rais wa Simba Sport Club Evans Aveva (Aliyekaa) Wakati wa Uzinduzi wa Tovuti ya Club Hiyo Anayeshuhudia ni Makamu wa Rais wa Club ya Simba Geofrey Nyange ‘Kaburu 
Simba Sports Club leo hiiimezindua tovuti yake Ili kukuza  mawasiliano  na  wadau wake mbalimbali  hususani; wanachama, wapenzi, vyombo  vya  habari na wadau wengine muhimu. 

Akizungumza  wakati  wauzinduzi  huo  Rais  wa  Simba Evans Aveva  alisema ‘’Katika dunia na zama  za  utandawazi  tovuti  ndio  na  mitandao   ya   jamii   ndio  njia  kuu ya mawasiliano. Sisi  tuliliona  hili  na  leo  hii  nafurahi  kuwa  Simba Sports Club itazindua  rasmi  tovuti  yake  ambayo  itakuwa  jukwaa  kuu la mawasiliano  na utoaji wa taarifa zake za  club ya   Simba. Natarajia wengi wenu mtaitumia kikamilifu na muhimu zaidi mtatupa mrejesho chanya kuhusu  tovuti yetu’’. 

Afisa Mtendaji Mkuuwa EAG Group Imani Kajula ambao ni washauri watekeleza ji wa Masokona Biashara wa Simba alisema ‘’Tovuti hii sio tuitaiwezesha Simba kuwapa wadau wake taarifa mbalimbalibali pia  itatumika  kwa  ajili  ya uuzaji  wa  vifaa  vya  Simba, Bidhaa  mbalimbali  mpya  na  muhimu  zaidi  kuwaunganisha   wanachama, mashabiki  na wapenzi wa  Simba  kutumia   mitandao  ya  jamii  iliyo   rasmi  ya  Simba Sports Club’’. 

Mkutano   huo  wa  wandishi  wa  habari   ulitumika  kutaarifu   Wanachama, Wapenzina  Vyombo   vya   habari   juu   ya  kocha   mpya   wa   Simba. Alizungumza  wakati  wakumtambulisha   kocha   mpya   wa   Simba, Rais   Aveva   alisema ‘’Baada ya kupitia  vyeti  na  maombi   ya  makocha   mbalimbali, Napenda  kuwa taarifu kuwa Klabu ya Simba imeingia  kwenye  mkataba  wa   kuifundisha   na   kocha Dylan Kerr raia   wa   Uingereza. Ni kocha   mwenye    uzoefu   wa   zaidi   ya   miaka 30, akiwa  amefanya  kazi  Nchi  mbalimbali  zikiwemo    Uingereza, Scotland, Vietnam   na    AfrikayaKusini’’.

MAKONDA KUHAMASISHA AJIRA KATIKA MICHEZO LEO


MH: PAUL MAKONDA MKUU WA WILAYA YA KINONDONI,
Anawaomba Wanakinondoni wote na wakazi wa DSM katika kuandaa maandalizi ya Team za Wilaya ya Kinondoni zitakazo kuwa na wachezaji watakao lipwa mshahara; katika:
1.Mpira wa miguu
(Football).
2.Netball.
3.Basketball.
Kushirikiana nae katika uzinduzi wa ligi hizo leo jumamosi, saa moja asubuhi Viwanja vya Leaders.
Ambapo  atazikabidhi Team 138 vifaa vya michezo.
SET 2  ZA JEZZY NA MIPIRA 2 KWA KILA TEAM.
WATAKUWAPO WATAALAMU WAKUPIMA AFYA ZA WACHEZAJI NA WATU WENGINE, KUTAKUWA PIA NA ZOEZI LA KUCHANGIA DAMU KWA ATAKAE PENDA.
TEAM ZOTE ZIKISHACHEZA KWA PAMOJA BAADAE WASHINDI  WATAUNDA  TEAM ZA WILAYA....
KWA MAELEZO ZAIDI FIKA VIWANJA VYA LEADERS MAPEMA leo(JMOS TAR 20 JUNE/2015) .
KIPAJI CHAKO AJIRA YAKO....
AJIRA SI BOMU.BOMU NI KUTOTUMIA KIPAJI CHAKO.
SERIKALI HAZIWEZI KUAJIRI WATU WOTE KATIKA AJIRA ZA OFISINI.
AJIRA INAJUMUISHA KUAJIRIWA NA KUJIAJIRI.NJOONI TUJIAJIRI TUPUNGUZE UGUMU WA MAISHA.
INAWEZEKANA...TUTIMIZE WAJIBU


Vifaa mbalimbali vya mchezo wa mpira wa kikapu vitakavyo kavidhiwa kwa Timu 138 na mkuu wa wilaya ya Kinindoni Ndg. Paulo akonda, ni pamoja na SET mbili  ZA JEZZY NA MIPIRA 2 KWA KILA TEAM.