Showing posts with label NEWS. Show all posts
Showing posts with label NEWS. Show all posts

Friday, July 1, 2016

TANZANIA INCREASES SIM-BANKING USERS BY 140%

Sim-banking users have increased by 140 percent in the first six months of this year, raising the bar of e-transaction in the country.



Sim-banking users have increased by 140 percent in the first six months of this year, raising the bar of e-transaction in the country.


The surge, from 250,000 users in 2015 to 600,000 as of yesterday, demonstrates that the country is walking towards e-payment, which boost revenue collection as it simplifies tax payment.

 “The number is climbing fast as more people have discovered the benefit of using Sim-banking and internet services,” CRDB Managing Director, Dr. Charles Kimei, said in Dar es Salaam.

He said the actual number is 1.6 million users but the rest are partially registered on Simbanking platform.

Dr. Kimei said at the moment the bank’s customers were around 2.5 million and they still educate the public on the advantage of using Simbanking and the risks of carrying hard-cash.

Monday, May 30, 2016

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI AONGOZA KIKAO CHA WAKUU WA ULINZI NA USALAMA TANZANIA

Mhandisi Massauni akitekeleza vyema wajibu wake katika kuboresha ufanisi wa wizara ya Mambo ya Ndani.

Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mh. Hamad Massauni (Mb) akiongoza kikao cha watendaji wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini Tanzania leo tarehe 30/05/2016. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Jeshi la polisi mjini Dodoma



Tuesday, May 3, 2016

KAMATI KUU YA CCM YAKUTANA NA KUFANYA MAAMUZI NYETI


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi imekutana April 03, 2016, Ikulu ya Chamwino, nje kidogo ya mji wa Dodoma.

Katika kikao hicho, Kamati Kuu pamoja na mambo mengine imefanya yafuatayo:-
Kamati Kuu imempongeza Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduizi kwa kura nyingi katika uchaguzi wa marudio uliofanyika tarehe 20 Machi, 2016 huko Zanzibar. Kamati Kuu pia imewapongeza wananchi wa Zanzibar kwa kuendelea kukiamini Chama Cha Mapinduzi kwa kukipa ushindi wa kishindo katika nafasi ya Rais, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani.

Aidha Kamati Kuu imepitisha majina ya Wabunge wa CCM 21 walioomba nafasi za Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa kupitia Wabunge wa CCM katika Bunge la Tanzania. Waliopitishwa ni:-

Ndugu Munde Tambwe Abdallah
Ndugu Jamal Kassim Ali
Ndugu Faida Mohamed Bakari
Ndugu Mbaraka Kitwana Dau
Ndugu Alex Raphael Gashaza
Ndugu Hawa Abdulrahaman Ghasia
Ndugu Ibrahim Hassanali Raza
Ndugu Angellah Jasmine Kairuki
Ndugu Dr.Hamis Andrea Kigwangalla
Ndugu Prof. Norman Sigalla King
Ndugu Livingstone Joseph Lusinde
Ndugu Dr. Angeline Sylester Mabula
Ndugu Almas Athuman Maige
Ndugu Angelina Adam Malembeka
Ndugu Agnes Mathew Marwa
Ndugu Yahaya Omary Massare
Ndugu Stephen Hirary Ngonyani
Ndugu Stanslaus Nyongo
Ndugu Mattar Ali Salum
Ndugu Peter Serukamba
Ndugu Hafidh Ali Tahir

Pia imepitisha majina kumi na tisa (19) ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi walioomba kugombea nafasi ya ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa kupitia Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Waliopitishwa ni:-

Ndugu. Mihayo Juma S. N'hunga
Ndugu Nassor Salim Ali
Ndugu Ali Khamis Bakari
Ndugu Salma Mussa Bilal
Ndugu Mgeni Hassan Juma
Ndugu Riziki Pemba Juma
Ndugu Yussuf Hassan Iddi
Ndugu Khadija Omar Kibano
Ndugu Shamata Shaaame Khamis
Ndugu Mmanga M. Mjawiri
Ndugu Dkt. Khalid Salum Mohamed
Ndugu Asha Abdalla Mussa
Ndugu Zulfa Mmaka omar
ndugu Hamad Abdalla Rashid
Ndugu Mohamed Ahmada Salum
Ndugu Harusi Said Suleiman
Ndugu Haroun Ali Suleiman
Ndugu Issa haji Ussi (Gavu)
Ndugu Bahati Khamis  Kombo

3   Kamati Kuu pia imepitisha majina ya Wabunge wa CCM wanne, walioomba  nafasi ya  Katibu wa kamati ya wabunge wote wa CCM.

Waliopitishwa ni :-
Mhe. Jason Samson Rweikiza
Mhe. Mary Pius Chatanda
Mhe. Mariam Nassoro Kisangi
Mhe. Abdala Hamis Ulega

Pia imepisha majina matatu ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi walioomba nafasi ya Katibu wa Kamati ya  wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa CCM

Waliopitishwa ni:-

Mhe. Ali Suleiman Ali (Shihata)
Mhe. Ali Salum Haji
Mhe. Abdallah Ali Kombo

4.  Katika kikao hicho pia Kamati Kuu imepitisha majina ya wanaCCM walioomba nafasi wazi mbalimbali za uongozi.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kibondo
Ndugu Josephat Mizozi Ntambindi
Ndugu Gilbert Ntausiga Kagoma
Ndugu Malck Daudi Rudugu

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa Wilaya ya Handeni
(i)  Ndugu Omar Abdallah Kigoda
(ii) Ndugu Maajabu Athuman Hamis
(iii) Ndugu Musssa Said Kidato
(iv) Ndugu Hamis Hamad Mnondwa
(v) Ndugu Athuman Yahaya Lukoya

(c )   Katibu wa Uchumi na Fedha, Mkoa wa Mbeya
(i) Ndugu Charles Michael Mwakipesile
(ii) Ndugu James Mwampondele Mwasunga
(iii) Ndugu Stephen Issac Mwakajumulo

(d)   Katibu wa Uchumi na Fedha, Mkoa wa Njombe
  (i) Ndugu Creiton Patric Lulambo
(ii) Ndugu Salu Batwel Sanga
(iii) Ndugu Reuben Erick Nyagawa

Imetolewa na:-

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Christopher Ole Sendeka
MSEMAJI WA CHAMA
CHAMA CHA MAPINDUZI
03/05/2016

Saturday, April 2, 2016

TANZANIA INAWEZA KUJIENDESHA BILA MISAADA TOKA NCHI WAHISANI



KUHUSU MCC KUSITISHA MSAADA WA MCC 2 NA SHUGHULI ZAKE TANZANIA: MTIZAMO

Nianze na nukuu hizi mbili kuntu za Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere- Mwenyezi Mungu amrehemu.

“Democracy is not a bottle of Coca-Cola which you can import. Democracy should develop according to that particular country”. June 1991 in Rio De Janeiro, Brazil

"Demokrasia sio chupa ya Coca-Cola ambayo unaweza kuagiza. Demokrasia lazima ikue na kuendelezwa kulingana na nchi husika". Juni 1991 Rio De Janeiro, Brazil (Tafsiri ni yangu)

“No nation has the right to make decisions for another nation; no people for another people”. From ‘A Peaceful New Year’ speech, Tanzania, January 1968

"Hakuna Taifa lina haki ya kufanya maamuzi juu ya Taifa lingine; wala watu juu ya watu wengine ". Hotuba ya Amani ya Mwaka Mpya, Tanzania, Januari 1968 (Tafsiri ni yangu)

Hili la Marekani na uamuzi wa MCC ni jambo la mpito na haliwezi kuua mahusiano yetu na Marekani. Tanzania na Marekani zinashirikiana kwa mambo mengi na MCC ni sehemu tu tena ni eneo jipya la ushirikiano. Uamuzi huu ni jaribio kwa uhuru wa Taifa letu. Hakuna namna nyingine ila kushinda hili kama tulivyoshinda mengine huko nyuma. Kwa wale ambao wameuona umri watakumbuka namna tulivunja uhusiano na Ujerumani Magharibi 1964 pale walipotaka kuwa na kauli hasi dhidi ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. 

Tulivunja uhusiano na Ujerumani Magharibi baada ya kutaka kuingilia Uhuru wa Mataifa Mawili huru yaliyoamua kuungana na kuunda Nchi Mpya ambayo leo tunajivunia, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 1965 Tulivunja uhusiano na Uingereza kufuatia na kitendo cha wazungu wachache kujitangazia Uhuru (Unilateral Declaration of Independence) kule Rhodesia na uingereza kukaa kimya na kushindwa kuchukua hatua stahiki. 

Tulivunja Uhusiano na Uingereza kuieleza Dunia kwamba Uhuru wa nchi za Afrika ni kipaumbele muhimu kwa Tanzania.  Jambo tunalopaswa kufahamu ni kuwa MCC 2 toka mwanzo imekuwa ni mtihani  dhidi ya uhuru wetu. Napenda ieleweke kwamba kipindi hiki kilichotokea sio kuvunjika kwa uhusiano wetu na Marekani bali taasisi ya MCC ndio imesitisha msaada wao kwetu, lakini mahusiano yetu na marekani bado yako pale pale, na si Marekani au Tanzania inayoweza kuugharimu uhusiano wetu.

MCC 1 ilikuwa ni chambo cha kutuvuta na tulipewa bila masharti tena hela nyingi dola milioni 698 na ni fedha tulizopewa moja kwa moja na kupewa uhuru wa kuamua tuzitumieje. Tanzania ilitakiwa kuainisha maeneo kisha wao wanatoa hela. Ndio maana miradi kama ile barabara ambazo hazikuwa zikipata ufadhili kwa kuwa hazikuonekana ni za kiuchumi na miradi ya maji ya Morogoro na kwingineko iliingizwa humu na kupata ufadhili. MCC 2 sio hivyo. Kwenye MCC 2 walengwa wakubwa ni sekta binafsi ya Marekani, hapa kuna mtego hapa, hapa ni biashara hapa. 

Mchakato wa MCC 2 ulipoanzishwa, wafanyabiashara kwa kushirikiana na Maseneta wakaanzisha hoja kuwa kwanini Marekani inatoa fedha kwa ufadhili katika nchi ambazo China ndio wenye kufaidika na fedha hizo? Wakaleta hoja ya kuwa Serikali ya Marekani ifanye jitihada ya kuweka fedha kwa kusaidia Sekta Binafsi ya Marekani kupenya Afrika. 

Ukaitishwa mkutano wa US-Africa Summit na agenda kubwa ikawa Power Africa. Katika Power Africa, Marekani ikalichagua eneo la Nishati (si uzalishaji viwanda) kwa kutambua kuwa ndio eneo pekee wanaloweza kushindana na wachina. Wakasema wataelekeza fedha huko kuisaidia Afrika kutatua tatizo la nishati ambalo ndio pembejeo ya viwanda. Wakaweka sharti kuwa fedha hizo na miradi hiyo itatekelezwa na Sekta Binafsi ya Marekani. 

Ndio sababu wengi wenu mtakumbuka hata Rais Obama alitangazia dhamira ile pale Ubungo kwenye Mitambo ya Symbion Power na sio kwamba alipenda kwenda kutembea Ubungo. Kuanzia hapo kumekuwepo na shinikizo kubwa sana na masharti magumu na yenye kuhamahama (shifting goal post) kutaka kuibaka sekta ya nishati nchini ikiwemo mageuzi ya TANESCO. Zikaainishwa hatua kadhaa,ambazo utekelezaji wake baadhi ni kisheria na kisera na hivyo haziwezi kwenda kwa deadline walizotaka. Kila bodi ikikutana wanaibua hiki na kile lakini wakisema hela watatoa. Hela hizi zikawa zimeshikiliwa kama chambo ukisogelea zinasogea, ni sawa na ule mchoro wa Mpanda Punde aliyeshika fimbo yenye majani na akiielekeza mbele ya punda, kwamba punda ataendelea kuyafuata majani akidhani atayafikia kumbe ndio anaupiga mwendo. Hatimaye wakasema wanasubiri uchaguzi mkuu jambo ambalo halihusiani na madai ya mwanzoni. Baada ya uchaguzi wakaibuka na suala la Zanzibar. 

Hivyo, uamuzi wao wa leo ni uamuzi uliotarajiwa. Pia ni uamuzi wenye madhara kwa sekta binafsi ya Marekani pia ambayo ndio ilikuwa itekeleze miradi hiyo. Kama Taifa ni muhimu kulinda utu na uhuru wetu. Ndio msingi wa sera yetu ya nje toka mwanzo na hata sasa. Tumetofautiana na Marekani katika hili tutapatana katika mengine. Ndio uhai wa maisha ya diplomasia. 

Wao nao wanayo hadhira ya wapiga kura wao wanayojaribu kuituliza huko nchini kwao kwa uamuzi huu. Tunapaswa kuheshimu uamuzi wao kama ambavyo wanapaswa kuuheshimu wetu. Hatimaye baadae tutapatana. Marekani inaihitaji Tanzania zaidi na Tanzania inaihitaji Marekani. Marekani inahitaji MCC 2 zaidi hali kadhalika Tanzania inahitaji MCC 2. 

Mahusiano ya Tanzania na Marekani hayakuanza na hayataisha na MCC. MCC imeyakuta na itayaacha. 

Kama marudio ya uchaguzi wa Zanzibar ndio kigezo, basi Marekani isingekuwa inatoa zaidi ya Dola Bilioni 3 kila mwaka kwa Egypt iliyo chini ya utawala wa kijeshi kwa sababu ya kuununua ugomvi wa Egypt na Israel na isingetoa kiasi cha dola bilioni 6 kwa Israel kila mwaka kwa yale wanayoyafanya dhidi ya Wapalestina. 

Huu ni wakati ambao Taifa linawaita Wazalendo wake. Wazalendo wasimame na kusema 'Nchi yangu KWANZA, iwe Sahihi au Imekosea" na Makuwadi watashangilia na kusema "si mnaona sasa kiko wapi?".

Huu ni wakati wa kujifunga mikanda na kulinda heshima yetu kama Taifa letu. Tuna vyanzo vya mapato vingi sana ambavyo hatujaanza kukusanya mapato, tuwe wabunifu na tusibweteke na kutegemea mapato yataongezeka maradufu kwa vyanzo vile vile.

Niseme kwa uchache, sababu walizotoa MCC, na ieleweke aliyetoa tamko ni MCC, heri lingetoka tamko hili Wizara ya Mambo ya Nje au Ikulu ya Marekani, moja ni Zanzibar na pili ni Sheria ya Makosa ya Mitandao (Cyber crimes Act).

Sasa hebu tujadili kidogo, hivi kule Zanzibar tulitaka kitokee nini pale ambapo wanasiasa walikuwa hawataki kujadiliana? Tume ile ile ya Uchaguzi ambayo bado ilikuwa na uhalali wa kikatiba na kisheria kuuitisha, kuufuta na kuuitisha tena uchaguzi ikachukua nafasi yake. Wanasiasa wasio makini wakaishia kuhamishia malumbano mitandaoni badala ya kuitafuta suluhu ya kisiasa na pale siasa iliposhindikana basi wangeitafuta suluhu katika mahakama za Zanzibar. Mezani wakashindwa, mahakamani hawakwenda. Tume ikachukua uongozi, uchaguzi ukaitishwa Wananchi wakapiga kura na sasa huko Zanzibar kuna serikali na baraza la wawakilishi. Hata mimi sifurahii sana njia waliyoichukua Zanzibar lakini ilibidi siasa za madaraka zisite ili tuanze kufanya siasa za maendeleo. Je wamarekani walitaka muujiza gani utokee huko.?

Kuhusu Sheria ya Mitandao, hata mimi siipendi, si twende mahakamani, bunge litaanza vikao muda si mrefu je wabunge si wapeleke hoja ya kuifanyia marekebisho sheria hii. Sasa Marekani (MCC) inapoweka shinikizo kwa suala la Sheria ambayo ni jambo la ndani na linaloweza kujadilika, sijaelewa. Mbona sie hatujapiga kelele Yule jamaa yao Trump alipotutusi waafrika na kusema sisi stahili yetu ni kuwekwa tena chini ya ukoloni (hapa nimechomekea tu).

INDHARI

Ni aibu kwa viongozi wa kisiasa kufurahia jambo hili, ni ishara ya ukuwadi wa kisiasa na ambao uko tayari kukumbatia mahusiano yanayotweza Uhuru wetu. It is now high time kufanya siasa safi za maendeleo (politics of development) na sio kujikita katika katika siasa za madaraka (Politics of Power).

Mwandishi, Ndg. Humphrey Polepole amenufaika na uelewa wa watu wenye uzoefu wa mahusiano ya Tanzania na nchi za Nje. Aidha, ni mnufaikaji (alumni) wa programu ya uongozi chini ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani.

Video ikielezea sababu za MCC kukataa kutimiza ahadi yake

Thursday, March 31, 2016

CHINA KUIMARISHA UHUSIANO NA TANZANIA


CHINA KUIMARISHA UHUSIANO NA TANZANIA



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. LU Youqing hii leo amefanya mazungumzo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Mh. January Makamba Ofisini kwa Waziri huyo Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo yao Balozi wa China amesema kuwa Serikali ya China inaamini kwamba uchaguzi wa Zanzibar uliofanyika mwishoni wa wiki iliyopita ulikuwa huru na haki. Balozi Youqing amesema kuwa Makamu wa Rais wa China ametuma salamu za pongezi kwa Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein kwa kuchaguliwa kwake na kwa watu wa Zanzibar kwa kuendesha uchaguzi huo katika misingi ya haki na uhuru. “Alikuwepo shuhuda wetu katika kushuhudia uchaguzi huo na alituambia kuwa ulikuwa wa haki na uhuru,” alisema Balozi huyo.

Katika mazungumzo hayo Balozi Youqing alisema Serikali ya China itaendelea kutoa misaada na kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwani huo ni wajibu wa mataifa makubwa kwa nchi zinazoendelea. Alimhakikishia Mheshimiwa Makamba kwamba China ina mipango mingi ya ushirikiano na Tanzania, ikiwemo kwenye sekta ya umeme na itaendelea kutoa ushirikiano kwa Tanzania, ikiwemo kupitia makampuni ya China, ili kuhakikisha malengo ya Tanzania kwenye sekta ya umeme yanatimia.

Kwa upande wake, Mheshimiwa Makamba alimshukuru Balozi Youqing pamoja na Serikali ya China kwa ushirikiano uliopo baina ya nchi hizo mbili. “Ujumbe na salamu ulizotoa leo umetupa faraja Watanzania. Urafiki baina ya nchi zetu, na baina ya vyama vyetu vya CCM na CCP, ni wa muda mrefu, ni wa majira yote, na umejengwa kwenye misingi ya kuheshimiana na hauna budi kuendelezwa”, alisema Mheshimiwa Makamba.

Pia Waziri Makamba na Balozi Youqing walikubaliana kutembelea Pemba na Unguja kwa pamoja mwezi Aprili ili kukagua na kutengeneza miradi ya maendeleo kati ya China na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Vilevile, walikubaliana kuhusu kutengeneza mradi mkubwa wa ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muugano wa Tanzania na China kwenye teknolojia zitakazosaidia kupunguza matumizi ya mkaa, hivyo kuhifadhi mazingira.

Waziri Makamba pia amemueleza Balozi Youqing kuhusu hitaji na umuhimu wa ushirikiano katika kuiwezesha Tanzania kumiliki teknolojia ya uzalishaji wa nishati kwa kutumia taka ngumu zinazozagaa katika miji ya Tanzania ambapo Balozi Youqing aliahidi kulifuatilia suala hilo. 



Sunday, March 20, 2016

Bw. KIKWETE AHUDHURIA MKUTANO KUJENGA SULUHU KWA NCHI YA LIBYA






Rais Mstaafu Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ndiye Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika katika utatuzi wa mgogoro wa Libya ameshiriki Mkutano wa Kamati ya Uandishi ya Baraza Maalum la Uandishi wa Katiba ya Libya (Constitution Drafting Assembly) unaoendelea mjini Salalah, Oman. Mkutano huo uliohudhuriwa pia na Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman, Mheshimiwa Yusuf bin Alawi bin Abdallah na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Martin Kobler.
Katika Mkutano huo, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ameelezea dhamira ya Umoja wa Afrika kuona kuwa mgogoro wa Libya unapatiwa suluhisho la kudumu. Amewakumbusha wajumbe wa mkutano huo kuwa jawabu la matatizo ya Libya ya hali ya usalama na changamoto zake liko mikononi mwao. Amewakumbusha dhamana kubwa iliyo juu yao na matarajio ya wananchi wa Libya kwa wajumbe hao kupawapatia Katiba ambayo itatoa majawabu kwa changamoto za Libya na kulinda haki na usawa kwa makundi yote.
Rais Mstaafu Kikwete pia amepongeza jitihada za Umoja wa Mataifa chini ya Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa Bw. Martin Kobler za kutafuta suluhu ya kudumu ya mgogoro wa Libya kupitia Mkataba wa Amani wa Libya (Libya Political Agreement) uliotiwa saini tarehe 17 Desemba, 2015 huko Shkirat, Morocco. Amehimiza wadau wa pande zote za siasa nchini Libya kutekeleza makubaliano hayo ikiwemo kuundwa kwa serikali na kusimikwa kwa serikali hiyo yalipo makao makuu ya nchi hiyo mjini Tripoli mapema iwezekanavyo.
Mwakilishi huyo wa Umoja wa Afrika amewahakikishia wajumbe hao utayari wa Umoja wa Afrika kufanya kazi kwa pamoja na Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Falme za Kiarabu (Arab League) na wadau wengine wote kusaidia jitihada za wananchi wa Libya kurejesha hali ya usalama, amani na utulivu nchini Libya.


Monday, February 22, 2016

TANZANIA BEGINS GENERATING ELECTRICITY FROM GEOTHERMAL RESOURCES TO PLUG THE SUPPLY DEFICIT


Tanzania is set to begin generating electricity from geothermal resources to plug the supply deficit.





Tanzania is set to begin generating electricity from geothermal resources to plug the supply deficit.
The Tanzania Geothermal Development Company (TGDC) is expected from June to start drilling three wells near Lake Ngozi in the southwestern the country as a first step to tap into underground geothermal steam.
Geothermal is a versatile energy form that can be used for a wide variety of direct applications such as spas, swimming pools, baths, heating greenhouses and dehydrating agricultural products.
Tanzania’s Energy Minister Sospeter Muhongo has directed TGDC to commence drilling of three geothermal wells near Lake Ngozi by June this year.
“We cannot continue waiting due to the shortage of power the country has been experiencing,” he said.
Tanzania wants to produce 200MW of geothermal power by 2020.
Studies have shown subsurface water temperatures of 230 to 250 degrees Celsius. The government will help TGDC to find funds for the Lake Ngozi project, including inviting in investors.
TGDC has identified 50 potential sites from where 5,000MW of geothermal electricity can be produced.

Thursday, February 4, 2016

FOLLOWING THE TANZANIAN GOVERNMENTAL ACTION, FINALY INDIAN GOVERIMENT TAKES CERTAIN MEASURES.





The Minister of Foreign Affair informed the Parliament of Tanzania about the quick governmental action following the Assault of its national in India.

The Ambassador of Tanzania in India briefly explain on the response towards ensuring safety and security of its nationals residing in india. 

SERIKALI YA TANZANIA YAINGILIA KUDHALILISHWA MWANAFUNZI WA KIKE BANGALORE INDIA

Serikali ya Tanzania yazungumzia tukio la mwanafunzi India

THURSDAY , 4TH FEB , 2016
Serikali imesema kuwa inaendelea kufatilia ili kuchukua hatia zaidi juu ya matukio yalitokea nchini India katika chuo cha Acharya Bangalore, ikiwemo la mwanafunzi wa Kike kudhalilishwa kwa kuvuliwa nguo.
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Agustino Maige
Akitoa tamko la Serikali leo Bunge Mjini Dodoma, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Agustino Maige amesema tayari serikali imeshapeleka dokezi la kidiplomasia kwa serikali ya india ili kuonyesha kukasirishwa na kitendo hicho.
Balozi Maige ameongeza kuwa tayari wameitaka serikali ya India kuchukua hatua za kipolisi kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo ikiwa ni pamoja na kupeleka ulinzi wa kutosha katika maeneo wanaoishi wanafunzi hususani wa kitanzania ambapo leo kumeri kwa mtu anaesadikiwa kuwa mtanzania kufariki katika mazingira ya kutatanisha.
Kwa upande wa baadhi ya wabunge wameiomba serikali kuwa na tamko rasmi la kuonyesha kuchukizwa na ubaguzi kwa watanzania pindi waendapo kuishi nje ya Tanzania.
Tukio hilo limekuja baada ya Gazeti la Deccan Chronical la Bangalore kuripoti kuwa tukio hilo limetokea baada ya mwanafunzi raia wa Sudan, Ismail Mohammed kugonga gari la raia mmoja wa india mkazi wa Hessaraghata aliekuwa na Mkewe na kusababisha kifo cha mama huyo.
Wakati huo huo Wanaume wanne wanaotuhumiwa kuhusika katika kumshambulia na kumvua nguo mwanafunzi wa kike kutoka Tanzania wamekamatwa, shirika la habari la AP limeripoti.
Waziri wa mashauri ya kigeni wa India Sushma Swaraj, aliandika kwenye Twitter kwamba amesikitishwa sana na “kisa hicho cha aibu” kilichotokea Jumapili eneo la Bangalore.

Saturday, January 30, 2016

MKUU WA MAJESHI Bw. DAVIS MWAMUNYANGE KUSTAAFU 2017.






RAIS John Magufuli amemwongeza mda wa mwaka mmoja, Mkuu wa  majeshi ya ulinzi nchini, Jenerali Davis Mwamunyange, ambaye alitakiwa kustaafu leo baada ya kutimiza umri  kwa mujibu wa katiba na sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mapema kwenye Makao makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) yaliyopo  Upanga jijini Dar es salaam, Jenerali Mwamunyange amesema leo alitakiwa kuungana na Brigedia wanne wa Jeshi ya ulinzi nchini  pamoja na Meja Jenerali wawili,  ambapo wote kwa  pamoja wamestaa ndani ya Jeshi kwa mujibu wa sheria ya jeshi hilo.

“Mimi mwenyewe ilikuwa nistaafu kazi leo tarehe 31 Januari,2016,lakini Rais na Amiri Jeshi mkuu ameamua kunibakiza katika utumishi jeshini kwa mwaka mmoja kuazia leo tarehe 31 januari, 2016 hadi tarehe  31 Januari 2017,” amesema Jenerali Mwamunyange.

Jeneral Mwamunyage amesema sababu iliyomfanya Rais Magufuli kumwongezea mda huo,imetokana na Rais kutopata mtu sahihi wa kujaza nafasi hiyo aliyonayo tena.
Hata hivyo, Jenerali Mwamunyange amesema Rais Magufuli amemteua  Luteni Jenerali Venance Mabeyo kuwa mnadhimu mkuu wa Jeshi la ulinzi la wananchi,

Sambamba na hilo, Jeneral Mwanunyange amesema pia, Rais Magufuli , amefanya uteuzi mkubwa ndani ya Jeshi hilo ili baada ya kuteua watu kushika nyadhifa mbali mbali ndani ya jeshi hilo,
    Jenerali Mwamunyange ametaja walioteuliwa na Rais, ni Meja Jenerali James Alois Mwakibolwa  kuwa Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la nchi Kavu, ambaye amechukua nafasi ya meja Jenerali Salum Mustafa Kijuu anayestaaafu kazi leo baada ya kufikisha umri wa kustaafu kisheria, ambapo Meja Mwakibolwa alikuwa ni mkuu wa tawi la utendaji wa kivita na mafunzo makao mkuu ya jeshi.

Jeneral Mwamunyange alimtaja pia aliyeteuliwa na Rais, ni -Meja Jenerali-Yakub Sirakwi kuwa  Mkuu wa chuo cha ulinzi wa Taifa (Commandant NDC) - kuchukua nafasi ya Meja Jenerali Gaudence Milanzi ambaye ameteuliwa na Rais kuwa Katibu mkuu wa wizara ya Maliasilia na utalii, Meja Jenerali Sirakwi alikuwa mratibu msaidizi mkuu baraza la usalama wa Taifa- BUT.

Mwengine aliyeteliwa na Rais Magufuli ni -Brigedia Jenerali George William Ingram, kuwa  Mkuu wa Kamandi ya jeshi la Anga, ambaye aliyechukua nafasi ya  Meja Jenerali Joseph Pwani aliyestaafu leo kisheria  baada ya kufikia umri wa kustaafu, Bregedia Jenerali Ingram alikuwa Afisa Mnadhimu katika mako makuu ya kamandi ya Jeshi la Anga.

 Pia Rais Magufuli alimteua Bregedia Jenerali M.W Isamuhyo kuwa  Mkuu wa jeshi la Kujenga Taifa-, kachukua nafasi ya Meja Jenerali Raphael Muhuga anayestaafu kazi leo, baada ya kufikisha umri wa kustaafu kazi kisheria, kabla ya uteuzi Bregedia Isamuhyo alikuwa mkurugenzi makao mkuu ya jeshi.

Vilevile Rais Magufuli amemteua Bregedia Jenerali Jacob Kingu  kuwa   mkuu wa shirika la mzinga-,kuchukua nafasi ya Meja Jenerali Charles Muzanila anayestaafu leo kisheria baada ya kufikisha umrii,Brigedia Jeneral Kingu alikuwa mkuu wa utawala na mafunzo katika makao mkuu ya jeshi la kujenga Taifa.

  Hata Hivyo,Rais Magufuli  amemteua Bregedia Jenerali Robison Mwanjela, kuwa mkuu wa chuo cha Tiba Lugalo (MCMS)- kuchukua nafasi ya Brigedia Jenerali Msangi anatestaafu leo kazi,baada ya kufikisha umri kustaafu kisheria,Kabla ya uteuzi Brigedia Jeneral Mwanjela alikuwa mkuu wa Tiba Hopsitali kuu ya Jeshi Lugalo.
   Aidha, Magufuli amemteua Brigedia Jeneral George Msongole kuwa   Kamanda wa Brigedia ya Tembo,- kuchukua nafasi ya Brigedia Jeneral J.M Chacha ambaye anastaafu leo baada kisheria baada ya kufikisha umri wa kustaafu,Bregedia Jenerali Msongole kabla ya kustaafu alikuwa bAfusa Mnadhimu makao makuu wa Jeshii.
  Rais Magufulia pia amemteua  Bregedia Jenerali Sylevesta M.Mijna kuwa mkuu wa chuo cha ukamanda  kuchukua nafasi ya Meja Jenerali Ezekiel Kyunga ambaye anastaafu kzai leo baada ya kufikisha umri wa kustaafu kisheria,ambapo kabya ya uteuzi,Bregedia Jenerali Minja alikuwa mkuu wa utawala katika chuo cha Ulinzii wa Taifa –NDC.

Tuesday, January 12, 2016

UVCCM YASHAURI AMANI KARUME KUVULIWA UWANACHAMA WA CCM

HOTUBA YA MWENYEKITI WA UMOJA WA VIJANA WA CCM  SADIFA J. KHAMIS AKIMKARIBISHA MAKAMU M/KITI WA CCM ZANZIBAR AMBAE PIA NI RAIS WA ZANZIBAR (MBLM) KATIKA KILELE CHA MATEMBEZI YA UVCCM KUADHIMISHA MIAKA 52 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR JUMATATU 11 JANUARI 2016.



Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye ni Makamu Mwenyekiti  wa CCM Zanzibar.  Dk Ali Mohamed Shein 
Mheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Balozi Seif Ali Idd.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM  Zanzibar  
Mama zetu wapendwa Mama  Mwanamwema Shein na Mama Asha Suleiman Idd.
Ndugu  Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM  Taifa 
Vijana kutoka katika maeneo mbalimbali Visiwani Zanzibar, Wazee, maveteran wa UVCCM , Waasisi  wetu  wageni waalikwa Mabibi na Mabwana .
Asalam  Aleykum.
Bwana Yesu Asifiwe.
Mheshimiwa Makamu Mwenyekiti

Leo tumekusanyika ikiwa imetimia miaka 52 tangu pale wazazi wetu walipoamua kwa dhamira moja ya kuukata mzizi wa fitna kwa kuudondosha utawala wa mabwenyenye na usultan uliovikalia visiwa vya Zanzibar toka mwaka 1804 hadi mwaka 1964.


Ndungu zangu, Kukusanyika kwetu hapa katika viwanja vya Maisara Suleiman tunalenga kukumbuka wazee  na  waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar kwa uamuzi wao wa kujitoa muhanga kwa ajili ya kupigania ukombozi wa nchi yetu, na hatimae kufanikisha mapinduzi matukufu.

Ndugu mgeni Rasmi, Tunapenda ifahamike kuwa jambo la kufanya Mapinduzi  halikuwa  jambo jepesi na rahisi kama inavyoonekana au kutaka kuchukuliwa na baadhi ya watu ambao sasa wanaonekana wamelishwa urojo na kuanza kusahau tulikotoka na kuanza kutamani kurejesha makovu ya ukoloni ambao wanataka kuurudisha kwa  mlango wa uani.

MSIMAMO WETU UVCCM
Sisi Vijana wa CCM, kwetu Mapinduzi yapo na yanaendelea ndani ya Chama na nje ya Chama, na sasa tunakitaka chama kwa sasa kukaa tayari kwa ajili ya mapinduzi makubwa ambayo yataendana na kauli mbiu yetu ya HAPA KAZI TU.

Aina ya watu na viongozi hao baadhi yao wako nje na ndani ya CCM. Wengine kati ya hao ni wale wenzetu ambao ndiyo  waliofaidi mno matunda ya Mapinduzi na sasa wamejivika ngozi ya usaliti  na kuwa maadui wa kuyayateketeza Mapinduzi yetu kwa kushirikiana na wakoloni wapya ambao ni maadui wa asili wa Mapinduzi ya Zanzibar. 

TAMKO LETU UVCCM 
Tunataka Tanzania isikie, Afrika itambue na dunia ijue kuwa UVCCM kwa sauti ya juu na umoja wetu tunatamka  wazi wazi kwamba viongozi wote wanaokihujumu chama na kutaka kurejesha utawala wa kikoloni visiwani Zanzibar VIONGOZI HAO TUNAWAJUA  na wao WANAJIJUA VIZURI NA WANATUSIKIA HIVI SASA, Tunataka dunia ijue na kila mmoja wetu hapa tulipo ajue. 

Sisi vijana tunatamka kwamba, tunachotaka kwanza ni usalama wa Chama chetu, uhai wa kudumu kwa Mapinduzi yetu matukufu, CCM KWANZA MTU BAADAE.
MHESHIMIWA MGENI RASMI KWA RUHUSA YAKO NAOMBA KUTUMBUA JIPU LEO, NA KUANZA LEO TUNAANZA SAFARI YA KUTUMBUA MAJIPU
Tunakitaka Chama chetu kuchukua hatua muhimu kama zile zilizochukuliwa mwaka 1987 wakati ambapo chama kilitumbua majipu ya aliyekuwa Waziri Kiongozi Seif Sharif Hamad na wenzake sita, akafuatia Mansoor Yussuf Himid , Hassan Nassor Moyo kwa kuvuliwa uanachama na kufukuzwa katika chama.
NA LEO KWA KAULI MOJA SISI VIJANA WA CCM TUNATAKA AVULIWE UANACHAMA NA KISHA AFUKUZWE MARA MOJA Amani Abeid Karume ndani ya CCM.

NARUDIA TENA 
NA LEO KWA KAULI MOJA SISI VIJANA WA CCM TUNATAKA AVULIWE UANACHAMA NA KISHA AFUKUZWE MARA MOJA Amani Abeid Karume ndani ya CCM.

Kwa sababu tumebaini ya kuwa yeye ni kirusi cha AMANI YETU, UMOJA WETU NA MSHIKAMANO  ndani ya Chama na sasa ni wakati wa kuweka ANTI-VIRIUSI

Ndugu Mgeni rasmi ieleweke kwamba miti siku zote haiwezi kuteketezwa na shoka bila kuanza kufanya ushirikiano au ushirika na mti ukawa mpini.
Amani Karume ameamua kuwa mpini unaoshirikiana na shoka ili kuteketeza na kukimaliza  Chama Cha Mapinduzi, sasa kabla hajakimaliza Chama basi ni wakati wa kumweka pembeni ili chama kisonge mbele.
Rai yetu kwako mheshimiwa mgeni rasmi, Kama mnaona na hamtaki kuchukua hatua za kinidhamu na kimaadili, sisi UVCCM tutatumia njia  nyingine  ya kufikisha kilio chetu bila aibu wala muhali.


Mapinduzi ya Zanzibar hayana nembo ya mtu, na si miliki ya  familia yoyote ya mtu,  bali ni urithi na tunu, halali za kila Mzanzibari na Mtanzania. Kuheshimu, kulinda na kuyaenzi Mapinduzi ni jukumu la kila mmoja wetu na si dhamana ya mtu mmoja.
Ndugu mgeni rasmi, ikumbukwe kuwa Ishara, vigezo na dalili za kuyaheshimu Mapinduzi matukufu, zinaoonekana bila ya mwanga wa tochi kwa mtu au kiongozi kadri inavyoonekana, anavyotenda na aina ya mwelekeo wa matendo yake, na ya familia yake na watoto wake . 

Kamwe, wananchama na viongozi Wanaoheshimu Mapinduzi yetu hawawezi kushirikiana na maadui wa Mapinduzi, Unapomuona mwenzenu au motto wake ameamua kushirikiana  na Mpinzani  wenu,  pika pakua , ahlan wasahlan bila kujali wala kukubali, hapo mjue sasa shoka limetiwa mpini na miti yote itateketea na ardhi kubaki jangwa.


Ndugu mgeni rasmi, Uamuzi wa kufanya Mapinduzi lilikuwa ni jambo la kufa au kupona. Hadi watu wanyonge wanapofikia  uamuzi  wa kufanya hivyo, aidha wamechoshwa na kukithiri kwa madhila, ukandamizaji, kunyimwa haki na usawa  , kukosa fursa mbali mbali katika nchi  yao ikiwemo na  kutopatiwa  huduma bora  za elimu ,afya, matibabu huku wakinyimwa  wasitumie rasilimali za nchi yao,  ardhi au kutokuwepo kwa uhuru wa kujitawala.
Miaka 52 iliopita waafrika katika Visiwa vyetu hawakuonekana binadamu wenye hadhi, heshima na hawastahili kupata jambo lolote lenye stahiki kama binadamu wengine.
Wapo viongozi ambao waliopewa nafasi za juu Serikalini wakachana  kumbukumbu  za vitabu, picha za historia za mateso walioyapata bibi, Babu , shangazi na mama zetu wakati wakitumikishwa kwenye kazi ngumu kwa maslahi ya kuutajirisha ukoloni wa ufalme.


Baada ya kutekeleza mradi wao huo wakapata sasa wanapigana hata historia ya kweli ya ukandamizaji na ubaguzi wa kikoloni usielezwe wala wanafunzi wasifundishwe mashuleni kwa madai kuwa kutarudisha chuki, hasira na hasama.
Wakati wao wakikataza jambo muhimu lisifanyike wanapita huko huko wakisema wanataka nchi yao, wanapigania uhuru wao jambo linalothibisha kwamba  hata mapinduzi yetu ambayo ndiyo uhuru na ukombozi wetu hawayatii na kuyaheshimu ipasavyo  .

Ndugu Mgeni rasmi. 
Naomba nitumie nafasi hii muhimu kuwaeleza kinagaubaga vijana wenzangu mahali popote walipo watambue kuwa wakoloni wote walioondoka katika nchi kadhaa za Afrika wamerudi kwao lakini wakoloni wa zanzibar bado wapo na wanakesha usiku na mchana kutaka kutupora Mapinduzi yetu. Wamepania kutupora kwa kushirikiana na mamluki waliomo ndani na nje ya chama chetu.

Sisi vijana wa UVCCM, Tunawaambia wale wote wanaojidanganya huku wakiota na kufikiria kwamba siku moja watatunyang'anya urithi wetu ili kuitawala tena nchi yetu. Jambo hilo nasema halitatokea na iwapo likitokea basi huyo mtawala ataitawala mikarafuu, minazi na miembe na si wanadamu.
Mheshimiwa Mgeni Rasmi, Leo sio siku ya hotuba kwangu naomba nichukue FURSA hii kutoa Shukrani kwa Mheshimiwa Rais kwa kukubali mwaliko wetu.
Shukrani kwa Mama Mwanamwema Shein kwa kukupa mawazo mazuri ya kutufikiria wanao kwa kila jambo.
Shukrani kwa Balozi Seif Ali Idd na mama Asha kwa busara na ushauri wa wao kwetu UVCCM.

Shukrani kwa Mhe. Otien Igogo Naibu Kamanda Mkuu – Bara kwa ushirikiano mzuri anaotuonyesha ndani ya Jumuiya yetu.
Shukrani kwa wake zangu wawili mama Salma Sadifa na Wastara kwa maliwazo na ushauri mzuri kwangu namna ya kuwaongoza UVCCM na Jimbo la Donge
Mwisho napenda kumshukuru kwa dhati kabisa Kaimu Katibu Mkuu Shaka Hamdu Shaka na Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM - Zanzibar Abdulghafari na Ndugu Kizigo Naibu Katibu Mkuu Bara kwa kazi kubwa na nzito wanayoifanya ya ndani ya UVCCM.

Naomba nichukue fursa hii adhimu kumualika Balozi Seif Ali Idd Naibu Kamanda Mkuu wa UVCCM Zanzibar, MZEE SHUPAVU NA MWELEDI, AMBAE KWETU TUNAMUONA NI MWAROBAINI AMBAO HATA KAMA NI MCHUNGU LAZIMA WAPINZANI WAUNYWE TU, aje hapa kwanza asalimie kisha uweze kukukaribisha wewe kuja kuzungumza na umati wa Vijana.

Karibu sana.
Ahsanteni sana kwa kunisikiliza.

Wednesday, December 23, 2015

MIHAYO N'HUNGA HAS BEEN AWARDED WITH LLB (Honours) AT ZANZIBAR UNIVERSITY DURING 2015 GRADUATION

Congratulations. Life has even better milestone for you.


So many dreamers; but only few achievers; and you are one of those who achieved the goal, you have come this far. There is no stopping now. Follow yourpassion, it will lead you to the fullfilment of your dreams. 
Congratulations on your graduation, we are very proud of you lil brother.
Mr. Mihayo N'hunga in a group photo with his parents,  Mrs. Tatu Juma (Mother); Mr. Juma S. N'hunga (Dad) and Mrs. Mwananisha Kudoja (Guardian -Mother)

Mr. Mihayo holding special presents from parents.

Mr. Mihayo receive a present from his sister Ms. Mwajuma as part of appreciations for graduation. 

Mr. Suleiman Juma (Uncle Sule) give a present to Mr. Mihayo during the graduation day, others are Ms. Mwajuma (Sister), Mr. Saidi (Brother), and Mrs Tatu Juma (Mother), during a happy moment at the University compound. 



Mr. Kudoja (Twin Brother), Mr. Mihayo and Mr. Mustafa Juma were also attended the graduation ceremony during which Mr. Mihayo wa awarded with LLB (Honours).





Sunday, November 8, 2015

UONGOZI WA CHADEMA MKOA WA RUKWA WAJIVUA KUFUATIA SINTOFAHAMU NDANI YA CHAMA HICHO

Aliyekuwa M/kiti wa Chadema wa mkoa wa Rukwa Bw Zeno Nkoswe

Viongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo mkoani Rukwa wameamua kuachia ngazi kwa kujiuzuru, ambapo mwenyekiti wa chama hicho na katibu wa mkoa huo pamoja na baraza zima la uongozi la mkoa wametangaza kuwa watabaki kuwa wanachama wa kawaida, kwa kile walichokidai kutoridhishwa na maamuzi ya makao makuu katika uteuzi wa nafasi ya ubunge wa viti maalumu kupitia chama hicho.
Akiongea na waandishi wa habari mjini Sumbawanga mwenyekiti wa Chadema wa mkoa wa Rukwa Bw Zeno Nkoswe, amesema licha ya kutoridhishwa na uteuzi wa Aida Kenani kuwa mbunge wa viti maalumu kutoka mkoa huo wa rukwa, pamoja na makao makuu ya chama kupewa taarifa mapema kuwa kiongozi huyo hivi sasa amekuwa msaliti, kwani mara tu baada ya kura za maoni amekuwa anakipigia debe chama cha TLP, lakini pia kutotekelezwa kwa ahadi ya kuwalipa mawakala zaidi ya 1,000 waliosimamia uchaguzi kwenye vituo mbalimbali, pia imekuwa sababu ya wao kujiuzuru nafasi zao.
 
Kwa upande wake katibu wa Chadema wa mkoa wa Rukwa Bw Ozem Chapita, akitoa ufafanuzi wa hatua hiyo amesema uteuzi wa mtu ambaye anaonekana ni msaliti, kunaweza kukaathiri hata uwezekano wa chama hicho kilichoshinda viti kumi kati ya tisa vya udiwani, kuweza kuiendesha halmashauri ya manispaa ya Sumbawanga kwa kuwa na meya wa manispaa, kwa kushindwa kupata kura za kutosha.



Tuesday, November 3, 2015

ORODHA YA WALIOSHINDA UBUNGE TANZANIA BARA



No.MBUNGEJIMBOCHAMA
1Dk Charles TizebaBuchosaCCM
2Nimrod MkonoButiamaCCM
3Omar BadwelChilonwaCCM
4Kanyasu JohnGeita MjiniCCM
5Pudensiana KikwembeKavuuCCM
6Sixtus MapundaMbinga MjiniCCM
7Hassan MasalaNachingweaCCM
8Abdallah ChikotaNanyambaCCM
9Richard MbogoNsimboCCM
10Ester MatikoTarime MjiniCHADEMA
11Mwakajoka FrankTundumaCHADEMA
12Joshua NassariArumeru MagharibiCHADEMA
13Dk Shukuru KawambwaBagamoyoCCM
14Andrew ChengeBariadi MagharibiCCM
15Oscar MukasaBiharamulo MagharibiCCM
16Wilfred LwakatareBukoba MjiniCHADEMA
17Jasson RwikizaBukoba VijijiniCCM
18Dotto BitekoBukombeCCM
19Eshter BulayaBunda MjiniCHADEMA
20Raphael ChegeniBusegaCCM
21Atupele MwakibeteBusekelo Rungwe MasharikiCCM
22Bilango SamsonBuyunguCHADEMA
23Ridhiwani KikweteChalinzeCCM
24Anthony MavundeDodoma MjiniCCM
25Freeman MboweHaiCHADEMA
26Mboni MhitaHandeniCCM
27Musa NtimiziIgalulaCCM
28Dk Dalaly KafumuIgungaCCM
29Musa Hassan ZunguIlalaCCM
30Janeth MbeneIlejeCCM
31Anjelina MabulaIlemelaCCM
32Mchungaji Peter MsigwaIringa MjiniCHADEMA
33William LukuviIsimaniCCM
34Njalu Daud SilangaItilima Bariadi Mashariki MkoaCCM
35Jumanne KishimbaKahama MjiniCCM
36Josephat KandegeKalamboCCM
37Godfrey MgimwaKalengaCCM
38Innocent BashangwaKaragweCCM
39Silvestry KokaKibaha MjiniCCM
40John Mnyika (Chadema)KibambaCHADEMA
41Ally Seif UngandoKibitiCCM
42Hasna MwilimaKigoma KusiniCCM
43Kigua OmariKilindiCCM
44Vinance MwamotoKiloloCCM
45Peter LijualikaliKilomberoCHADEMA
46Vedasto EdgerKilwa KaskaziniCUF
47Saidi BungaraKilwa KusiniCUF
48Luhaga MpinaKisesaCCM
49Suleman NchambiKishapuCCM
50Emmanuel PapianKitetoCCM
51Edwin SandaKondoa MjiniCCM
52Stephen NgonyaniKorogwe VijijiniCCM
53Mary ChatandaKorogwe MjiniCCM
54Shanif MansoorKwimbaCCM
55Dk Harrison MwakyembeKyelaCCM
56Innocent BilakwateKyerwaCCM
57Zubery KuchaukaLiwaleCUF
58Onesmo ole NangoleLongidoCHADEMA
59Victor MwambalaswaLupaCCM
60Cosato ChumiMafinga MjiniCCM
61Boniventura DesteryMaguCCM
62Dk Norman SigalaMaketeCCM
63Seif GulamaliManongaCCM
64Mashimba NdakiMaswa MagharibiCCM
65Stanslaus NyongoMaswa MasharikiCCM
66Mangungu AliMbagalaCCM
67Aroon MullaMbaraliCCM
68Joseph MbilinyiMbeya MjiniCHADEMA
69Augustino MaseleMbogweCCM
70Zacharia Paul IsaayMbuluCCM
71Hassan Hassan BabaliMchingaCUF
72Salum KhamisMeatuCCM
73Joseph HauleMikumiCHADEMA
74Charles KitwangaMisungwiCCM
75Dustan KitandulaMkingaCCM
76Abdallah UlegaMkurangaCCM
77Rashidi ShangazMlaloCCM
78Susana KiwangaMlimbaCHADEMA
79Julius KalangaMonduliCHADEMA
80Mgumba OmariMorogoro KusiniMasharikiCCM
81Anthony KomuMoshi VijijiniCHADEMA
82George LubelejeMpwapwaCCM
83Ezekiel MaigeMsalalaCCM
84Nape NnauyeMtamaCCM
85Livingstone LusindeMteraCCM
86Hawa GhasiaMtwara VijijiniCCM
87Mahamoud MgimwaMufindi KaskaziniCCM
88Mendrad KigolaMufindi KusiniCCM
89Atashasta NditiyeMuhambweCCM
90Rajab AdadiMuhezaCCM
91Charles MwijageMuleba KaskaziniCCM
92Pro Anna TibaijukaMuleba KusiniCCM
93Vedastus MathayoMusoma MjiniCCM
94Prof Sospeter MuhongoMusoma VijijiniCCM
95Prof Jumanne MaghembeMwangaCCM
96Kangi LugolaMwibaraCCM
97Dua NkurumaNanyumbuCCM
98Cesil MwambeNdandaCHADEMA
99George Mkuchika (CCM)Newala MjiniCCM
100Alex Rafael GashazaNgaraCCM
101Joram HongoliNjombe KaskaziniCCM
102Ally MohamediNkasi KaskaziniCCM
103Desderius MipataNkasi KusiniCCM
104Dk Diodorus KamalaNkengeCCM
105Stanslaus MabulaNyamaganaCCM
106Hussein KassuNyangwaleCCM
107Hussein BasheNzega MjiniCCM
108Jumaa AwesoPanganiCCM
109Jenista MhagamaPeramihoCCM
110Joseph Selasini (Chadema)RomboCHADEMA
111Mohamed MchengerwaRufijiCCM
112Saul AmonRungwe MagharibiCCM
113Dk Mathayo DavidSame MagharibiCCM
114Naghenjwa KaboyokaSame MasharikiCHADEMA
115William NgerejaSengeremaCCM
116Steven MaseleShinyanga MjiniCCM
117Joseph KakundaSikongeCCM
118Tundu LissuSingida MasharikiCHADEMA
119Ahmed SalumSolwaCCM
120Leonidas GamaSongea MjiniCCM
121Aeshi HilalySumbawanga MjiniCCM
122Richard NdasaSumveCCM
123Almas MaigeTabora KaskaziniCCM
124Emmanuel MwakasakaTabora MjiniCCM
125Abdallah MtoleaTemekeCUF
126Ramo MakaniTunduru KaskaziniCCM
127Daimu MpakateTunduru KusiniCCM
128Saed KubeneaUbungoCHADEMA
129Joseph MkundiUkereweCHADEMA
130Waitara MwitaUkongaCHADEMA
131Magreth SittaUrambo MasharikiCCM
132James MbatiaVunjoNCCR-Mageuzi
133Japhet HasungaVwawaCCM
134Gipson Ole MeseyekiArumeru MagharibiCHADEMA
135Joshua NassariArumeru MasharikiCHADEMA
136Pauline GekulBabati MjiniCHADEMA
137Jitu Vrajlal SonBabati VijijiniCCM
138Albert ObamaBuhingweCCM
139January MakambaBumbuliCCM
140Boniphace MwitaBunda VijijiniCCM
141Lolesia BukwimbaBusandaCCM
142Dr Merdad Kalemani ChananjaChatoCCM
143Juma NkamiaChembaCCM
144Ahmed ShabibyGairoCCM
145Joseph MusukumaGeita VijijiniCCM
146Mary NaguHanangCCM
147Magdalena SakayaKaliuaCUF
148Willy QambaloKaratuCHADEMA
149Daniel NsanzugwankoKasulu MjiniCCM
150Holle VumaKasulu VijijiniCCM
151Hamoud JumaaKibaha VijijiniCCM
152George SimbachaweneKibakweCCM
153Peter SerukambaKigoma KaskaziniCCM
154Zitto KabweKigoma MjiniACT
155Bawasili MbarakaKilosa KatiCCM
156Suleiman JaffoKisaraweCCM
157Dk Ashatu KijajiKONDOA VIJINICCM
158Job NdugaiKongwaCCM
159Hassan SelemanLindi UrbanCCM
160Kitwana DauMafiaCCM
161Dk Haji MpondaMalinyiCCM
162Manase NjezaMbeya VijijiniCCM
163Martin MsuhaMbinga RuralCCM
164Pascal HaongaMboziCHADEMA
165Flatey Gregory MassayMbulu VijijiniCCM
166Mhandisi KamweleMleleCCM
167David SilindeMombaCHADEMA
168Mbena JosephMorogoro KusiniCCM
169AbdulaAziz AboodMorogoro MjiniCCM
170Jaffar MichaelMoshi MjiniCHADEMA
171Sebastian KapufiMpanda MjiniCCM
172Moshi KakosoMpanda vijijiniCCM
173Maftaah NachumaMtwara MjiniCUF
174Suleiman Saddiq MuradMvomeroCCM
175Rashid AkbalNewala VijijiniCCM
176William Ole NashaNgorongoroCCM
177Edward MwalongoNjombe UrbanCCM
178Dr Khamis Kigwangalla (CCM)Nzega VijijiniCCM
179Lameck AiroRoryaCCM
180Kassim MajaliwaRuangwaCCM
181Marwa RyobaSerengetiCHADEMA
182Dk Godwin MollelSihaCHADEMA
183James Ole MillyaSimanjiroCHADEMA
184Philipo MulugoSongweCCM
185Ahmad KataniTandahimbaCUF
186Mussa MbaroukTanga MjiniCUF
187John HecheTarime Vijijini