Showing posts with label POLITICS. Show all posts
Showing posts with label POLITICS. Show all posts

Tuesday, January 12, 2016

UVCCM YASHAURI AMANI KARUME KUVULIWA UWANACHAMA WA CCM

HOTUBA YA MWENYEKITI WA UMOJA WA VIJANA WA CCM  SADIFA J. KHAMIS AKIMKARIBISHA MAKAMU M/KITI WA CCM ZANZIBAR AMBAE PIA NI RAIS WA ZANZIBAR (MBLM) KATIKA KILELE CHA MATEMBEZI YA UVCCM KUADHIMISHA MIAKA 52 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR JUMATATU 11 JANUARI 2016.



Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye ni Makamu Mwenyekiti  wa CCM Zanzibar.  Dk Ali Mohamed Shein 
Mheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Balozi Seif Ali Idd.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM  Zanzibar  
Mama zetu wapendwa Mama  Mwanamwema Shein na Mama Asha Suleiman Idd.
Ndugu  Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM  Taifa 
Vijana kutoka katika maeneo mbalimbali Visiwani Zanzibar, Wazee, maveteran wa UVCCM , Waasisi  wetu  wageni waalikwa Mabibi na Mabwana .
Asalam  Aleykum.
Bwana Yesu Asifiwe.
Mheshimiwa Makamu Mwenyekiti

Leo tumekusanyika ikiwa imetimia miaka 52 tangu pale wazazi wetu walipoamua kwa dhamira moja ya kuukata mzizi wa fitna kwa kuudondosha utawala wa mabwenyenye na usultan uliovikalia visiwa vya Zanzibar toka mwaka 1804 hadi mwaka 1964.


Ndungu zangu, Kukusanyika kwetu hapa katika viwanja vya Maisara Suleiman tunalenga kukumbuka wazee  na  waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar kwa uamuzi wao wa kujitoa muhanga kwa ajili ya kupigania ukombozi wa nchi yetu, na hatimae kufanikisha mapinduzi matukufu.

Ndugu mgeni Rasmi, Tunapenda ifahamike kuwa jambo la kufanya Mapinduzi  halikuwa  jambo jepesi na rahisi kama inavyoonekana au kutaka kuchukuliwa na baadhi ya watu ambao sasa wanaonekana wamelishwa urojo na kuanza kusahau tulikotoka na kuanza kutamani kurejesha makovu ya ukoloni ambao wanataka kuurudisha kwa  mlango wa uani.

MSIMAMO WETU UVCCM
Sisi Vijana wa CCM, kwetu Mapinduzi yapo na yanaendelea ndani ya Chama na nje ya Chama, na sasa tunakitaka chama kwa sasa kukaa tayari kwa ajili ya mapinduzi makubwa ambayo yataendana na kauli mbiu yetu ya HAPA KAZI TU.

Aina ya watu na viongozi hao baadhi yao wako nje na ndani ya CCM. Wengine kati ya hao ni wale wenzetu ambao ndiyo  waliofaidi mno matunda ya Mapinduzi na sasa wamejivika ngozi ya usaliti  na kuwa maadui wa kuyayateketeza Mapinduzi yetu kwa kushirikiana na wakoloni wapya ambao ni maadui wa asili wa Mapinduzi ya Zanzibar. 

TAMKO LETU UVCCM 
Tunataka Tanzania isikie, Afrika itambue na dunia ijue kuwa UVCCM kwa sauti ya juu na umoja wetu tunatamka  wazi wazi kwamba viongozi wote wanaokihujumu chama na kutaka kurejesha utawala wa kikoloni visiwani Zanzibar VIONGOZI HAO TUNAWAJUA  na wao WANAJIJUA VIZURI NA WANATUSIKIA HIVI SASA, Tunataka dunia ijue na kila mmoja wetu hapa tulipo ajue. 

Sisi vijana tunatamka kwamba, tunachotaka kwanza ni usalama wa Chama chetu, uhai wa kudumu kwa Mapinduzi yetu matukufu, CCM KWANZA MTU BAADAE.
MHESHIMIWA MGENI RASMI KWA RUHUSA YAKO NAOMBA KUTUMBUA JIPU LEO, NA KUANZA LEO TUNAANZA SAFARI YA KUTUMBUA MAJIPU
Tunakitaka Chama chetu kuchukua hatua muhimu kama zile zilizochukuliwa mwaka 1987 wakati ambapo chama kilitumbua majipu ya aliyekuwa Waziri Kiongozi Seif Sharif Hamad na wenzake sita, akafuatia Mansoor Yussuf Himid , Hassan Nassor Moyo kwa kuvuliwa uanachama na kufukuzwa katika chama.
NA LEO KWA KAULI MOJA SISI VIJANA WA CCM TUNATAKA AVULIWE UANACHAMA NA KISHA AFUKUZWE MARA MOJA Amani Abeid Karume ndani ya CCM.

NARUDIA TENA 
NA LEO KWA KAULI MOJA SISI VIJANA WA CCM TUNATAKA AVULIWE UANACHAMA NA KISHA AFUKUZWE MARA MOJA Amani Abeid Karume ndani ya CCM.

Kwa sababu tumebaini ya kuwa yeye ni kirusi cha AMANI YETU, UMOJA WETU NA MSHIKAMANO  ndani ya Chama na sasa ni wakati wa kuweka ANTI-VIRIUSI

Ndugu Mgeni rasmi ieleweke kwamba miti siku zote haiwezi kuteketezwa na shoka bila kuanza kufanya ushirikiano au ushirika na mti ukawa mpini.
Amani Karume ameamua kuwa mpini unaoshirikiana na shoka ili kuteketeza na kukimaliza  Chama Cha Mapinduzi, sasa kabla hajakimaliza Chama basi ni wakati wa kumweka pembeni ili chama kisonge mbele.
Rai yetu kwako mheshimiwa mgeni rasmi, Kama mnaona na hamtaki kuchukua hatua za kinidhamu na kimaadili, sisi UVCCM tutatumia njia  nyingine  ya kufikisha kilio chetu bila aibu wala muhali.


Mapinduzi ya Zanzibar hayana nembo ya mtu, na si miliki ya  familia yoyote ya mtu,  bali ni urithi na tunu, halali za kila Mzanzibari na Mtanzania. Kuheshimu, kulinda na kuyaenzi Mapinduzi ni jukumu la kila mmoja wetu na si dhamana ya mtu mmoja.
Ndugu mgeni rasmi, ikumbukwe kuwa Ishara, vigezo na dalili za kuyaheshimu Mapinduzi matukufu, zinaoonekana bila ya mwanga wa tochi kwa mtu au kiongozi kadri inavyoonekana, anavyotenda na aina ya mwelekeo wa matendo yake, na ya familia yake na watoto wake . 

Kamwe, wananchama na viongozi Wanaoheshimu Mapinduzi yetu hawawezi kushirikiana na maadui wa Mapinduzi, Unapomuona mwenzenu au motto wake ameamua kushirikiana  na Mpinzani  wenu,  pika pakua , ahlan wasahlan bila kujali wala kukubali, hapo mjue sasa shoka limetiwa mpini na miti yote itateketea na ardhi kubaki jangwa.


Ndugu mgeni rasmi, Uamuzi wa kufanya Mapinduzi lilikuwa ni jambo la kufa au kupona. Hadi watu wanyonge wanapofikia  uamuzi  wa kufanya hivyo, aidha wamechoshwa na kukithiri kwa madhila, ukandamizaji, kunyimwa haki na usawa  , kukosa fursa mbali mbali katika nchi  yao ikiwemo na  kutopatiwa  huduma bora  za elimu ,afya, matibabu huku wakinyimwa  wasitumie rasilimali za nchi yao,  ardhi au kutokuwepo kwa uhuru wa kujitawala.
Miaka 52 iliopita waafrika katika Visiwa vyetu hawakuonekana binadamu wenye hadhi, heshima na hawastahili kupata jambo lolote lenye stahiki kama binadamu wengine.
Wapo viongozi ambao waliopewa nafasi za juu Serikalini wakachana  kumbukumbu  za vitabu, picha za historia za mateso walioyapata bibi, Babu , shangazi na mama zetu wakati wakitumikishwa kwenye kazi ngumu kwa maslahi ya kuutajirisha ukoloni wa ufalme.


Baada ya kutekeleza mradi wao huo wakapata sasa wanapigana hata historia ya kweli ya ukandamizaji na ubaguzi wa kikoloni usielezwe wala wanafunzi wasifundishwe mashuleni kwa madai kuwa kutarudisha chuki, hasira na hasama.
Wakati wao wakikataza jambo muhimu lisifanyike wanapita huko huko wakisema wanataka nchi yao, wanapigania uhuru wao jambo linalothibisha kwamba  hata mapinduzi yetu ambayo ndiyo uhuru na ukombozi wetu hawayatii na kuyaheshimu ipasavyo  .

Ndugu Mgeni rasmi. 
Naomba nitumie nafasi hii muhimu kuwaeleza kinagaubaga vijana wenzangu mahali popote walipo watambue kuwa wakoloni wote walioondoka katika nchi kadhaa za Afrika wamerudi kwao lakini wakoloni wa zanzibar bado wapo na wanakesha usiku na mchana kutaka kutupora Mapinduzi yetu. Wamepania kutupora kwa kushirikiana na mamluki waliomo ndani na nje ya chama chetu.

Sisi vijana wa UVCCM, Tunawaambia wale wote wanaojidanganya huku wakiota na kufikiria kwamba siku moja watatunyang'anya urithi wetu ili kuitawala tena nchi yetu. Jambo hilo nasema halitatokea na iwapo likitokea basi huyo mtawala ataitawala mikarafuu, minazi na miembe na si wanadamu.
Mheshimiwa Mgeni Rasmi, Leo sio siku ya hotuba kwangu naomba nichukue FURSA hii kutoa Shukrani kwa Mheshimiwa Rais kwa kukubali mwaliko wetu.
Shukrani kwa Mama Mwanamwema Shein kwa kukupa mawazo mazuri ya kutufikiria wanao kwa kila jambo.
Shukrani kwa Balozi Seif Ali Idd na mama Asha kwa busara na ushauri wa wao kwetu UVCCM.

Shukrani kwa Mhe. Otien Igogo Naibu Kamanda Mkuu – Bara kwa ushirikiano mzuri anaotuonyesha ndani ya Jumuiya yetu.
Shukrani kwa wake zangu wawili mama Salma Sadifa na Wastara kwa maliwazo na ushauri mzuri kwangu namna ya kuwaongoza UVCCM na Jimbo la Donge
Mwisho napenda kumshukuru kwa dhati kabisa Kaimu Katibu Mkuu Shaka Hamdu Shaka na Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM - Zanzibar Abdulghafari na Ndugu Kizigo Naibu Katibu Mkuu Bara kwa kazi kubwa na nzito wanayoifanya ya ndani ya UVCCM.

Naomba nichukue fursa hii adhimu kumualika Balozi Seif Ali Idd Naibu Kamanda Mkuu wa UVCCM Zanzibar, MZEE SHUPAVU NA MWELEDI, AMBAE KWETU TUNAMUONA NI MWAROBAINI AMBAO HATA KAMA NI MCHUNGU LAZIMA WAPINZANI WAUNYWE TU, aje hapa kwanza asalimie kisha uweze kukukaribisha wewe kuja kuzungumza na umati wa Vijana.

Karibu sana.
Ahsanteni sana kwa kunisikiliza.

Tuesday, October 13, 2015

BAADA YA UHAKIKI WATU 7,743 KUTOPIGA KURA HUKO ZANZIBAR

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Mh. Jecha Salim Jecha akiwasilisha Taarifa kuhusu maandalizi ya uchaguzi Mkuu 2015


Zanzibar: Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imesema mchakato mzima wa kuhakiki taarifa katika Daftar la Kudumu la wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktobar 25 mwaka huu 2015 umeshakamilika huku watu 7,743, watakosa nafasi ya kupiga kura kwa kukosa sifa.
Akitoa taarifa ya maandalizi ya uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu 2015 kwa wadau wa uchaguzi Zanzibar Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jecha Salim, huko katika ukumbi wa Bwawani Hotel Mjini Unguja, amesema kuwa mchakato wa kuhakiki taarifa za wapiga kura umeshakamilika baada ya kukamilika kwa uandikishaji wapya katika Daftari hilo.
Jecha alisema kuwa jumla ya wapiga kura 503,860, wametimiza masharti kuwa wapiga kura katika Uchaguzi Mkuu Mwaka huu, huku watu 7,743 wamefutwa katika Daftar la wapiga kura kutokana na kukosa sifa za kuwamo katika Daftari hilo.
“Kwa sasa hatua kubwa za utayarishaji na uchambuzi juu ya Daftari la wapiga kura zimekamilika ambapo jumla ya wapiga kura 503,860 watapata nafasi ya kuchagua viongozi wawatakao na 7,743, watakosa nafasi ya kuchagua kwa mwaka huu kutokana na kukosa sifa kisheria”alisema Jecha.
Hata hivyo Jecha alisema kuwa Tume ya Uchaguzi kwa sasa imekamilisha uchapishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, ambapo ni matarajio yao kuwa kuanza kulibandika katika vituo vyote vya Unguja na Pemba.
Alifahamisha kuwa kazi ya ubandikaji wa majina yaliomo katika daftari hilo Tume ya Uchaguzi imepanga kuanzia tarehe 18 Oktoba 2015 kwa ajili ya kuwapa nafasi nzuri wananchi ili waweze kutazama majina yao kwa utulivu.
Jecha alisema kuwa jumla ya maeneo ya uchaguzi 380 pamoja na vituo 1,580 vya uchaguzi vinatarajiwa kubandikwa majina hayo ambapo kila kituo cha kupigia kura kitakuwa na wapiga kura 350.
“Wastani wa wapiga kura kwa kila kituo 350 ila katika mazingira maalum baadhi ya vituo vinaweza kuzidi kufikia 399, na kwa vyovyote vile hakutakuwa na kituo kitakachokuwa chini ya idadi ya wapiga kura 50”alisema Jecha.
Aliongezea kwa kusema kuwa “Tumetoa taarifa kwa kila Chama Cha Siasa kilichoweka mgombea wa Urais, kuja kuchukua Daftari hilo la wapiga kura kwa ajili ya kutumia siku ya uchaguzi kwa kuwapa mawakala wao”.
Jecha alisema kuwa kwa upande wa Tume ya Uchaguz hivi sasa mambo mengi tayari wamekamilisha ikiwamo vifaa vya kupigia kura pamoja na miongozo, kanuni na maadili ya Uchaguzi.
Kwa upande matayarisho ya upigaji kura Jecha alisema kuwa Tume imepanga kusambaza vifaa vya Uchaguzi siku ya tarehe 24 / 10/ 2015 kuanzia saa nane mchana kwa vituo vyote vya Uchaguzi,usambazaji ambao utafanywa kati ya viongozi wa tume na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).
Alifahamisha kuwa siku ya upigaji kura vituo vitaanza kufunguliwa saa moja kamili (1.00) asubuhi na kufungwa saa kumi jioni (10:00) ya siku hiyo hiyo ya tarehe 25 ya Oktoba 2015.
Baada ya hatua hiyo kitakachofuata ni uhisabuji wa kura za wagombea ambapo Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo atafanya majumuisho ya kura ndani ya Jimbo na mara baada ya kukamilika Msimamizi huyo atatangaza matokeo ya Uchaguzi kwa ngazi ya Mwakilishi na Udiwani tu.
Huku matokeo ya Urais Msimamizi huyo wa Uchaguzi Jimbo atafanya majumuisho ya kura na atabandika nakala ya matokeo hayo katika ukuta ili wananchi wapate nafasi ya kuona matokeo hayo.
“Mara baada ya kukamilika kwa majumuisho Msimamizi wa Uchaguzi atampatia kila Wakala fomu moja ya mtokeo husika, huku Tume ya Uchaguzi ikibaki na kazi ya kutangaza matokeo ya Uchaguzi kwa kila Jimbo mara baada ya kufanyiwa uhakiki wa matokeo kutoka kwa wasimamizi Uchaguzi” alisema.
Jecha alisema kuwa karatasi za kupigia kura zitakazotumika katika Uchaguzi wa mwaka huu 2015 zimechapishwa kutoka nchini Afrika ya Kusini chini ya kampuni ya Bidvest-Lithotech.
Harakati zote zinazofanywa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ya uendeshaji wa Uchaguzi mwaka huu zipo chini ya Mfuko wa Serikali ya Zanzibar ambapo mwaka huu Serikali imetenga jumla ya shilling bilioni 7.5, ambapo hadi sasa Tume imeshaingiziwa shilling bilioni 2.5.

Tuesday, September 29, 2015

CHADEMA WAENDELEA KUDHALILIKA KUTOKANA NA SABABU ZA KUHAIRISHA MIKUTANO YAO YA KAMPENI

CHADEMA WAENDELEA KUDHALILIKA KUTOKANA NA SABABU ZA KUHAIRISHA MIKUTANO YAO YA KAMPENI

Taarifa ya wazi kwa umma kufuatia taarifa ya CHADEMA kuhairisha mkutano


Hii ni baada ya kuhairishwa mkutano wa kampeni za CHADEMA/ UKAWA mjini Tanga ambapo taarifa za ndani za chama hicho zilisema kuwa mkutano huo ulihairishwa kutokana na wimbi kubwa la wanachama waliojitokeza katika viwqnja vya Tangamano jambo lililosababisha kushindwa kutua kwa Helkopta ya mgombea Urais wa chama hicho Edward N. Lowassa, ambapo ililazimika kwenda kutua uwanja wa ndege na ndipo mgombea huyo na msafara wake walifika viwanjani hapo kwa kutumia gari ziizoandaliwa kwa ajili yao. Taarifa hiyo ilieleza kwamba katika mkutano huo mkubwa sana kulikua na msongamano mkubwa uliosababisha wanachama wengi kuanguka na kupoteza fahamu (kuzimia) ambapo kitengo cha huduma ya kwanza kushindwa kumudu hali hiyo licha ya wagonjwa wengi kufikishwa hospitali mbalimbali. Hata hivyo katika mkutano huo mgombea huo wa Urais alihutubia umma huo kwa tariba dakika tatu tu kabla ya kuhairishwa na mgombea huyo kuwahishwa haraka katika dharura iliyomlazimu kuondoka uwanjani hapo. 



Sunday, September 27, 2015

N'HUNGA AZIDI KUIHAKIKISHIA USHINDI KWA CCM JIMBO LA MWERA ZANZIBAR

N'HUNGA AZIDI KUHAKIKISHA USHINDI KWA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)


Mgombea Uwakilishi jimbo la Mwera akielezea utekelezaji wa Ilani na mpango mkakati unaolenga kuharakisha maendeleo kwa wananchi jimboni hapo.


Wagombea nafasi za Ubunge, Uwakilishi na Udiwani jimbo la Mwera wakifanya dua maalum kuomba amani muda mfupi kabla ya kuanza mkutano wa kampeni uliofanyika katika tawi la CCM la Mwera.
Diwani wa WADI ya Mwera Bi Shani akimnadi mgombea Uwakilishi Bw. Mihayo N'hunga wakati wa mkutano wa kampeni hizo katika viwanja vya Tawi la CCM Mwera mapema leo. 

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM mkoa wa Mbeya Bi. Fatma akiwatambulisha na kuwanadi wagombea wa nafasi mbalimbali jimbo la mwera wakati wa kampeni hizo.

Bw. Mihayo N'hunga akimtambulisha na kumuombea kura mgombea Udiwani wa Wadi ya Kianga Bw. Seleman Abbas (Gobo) katika kampeni hizo.

Mgombea Ubunge Bw. Makame Khamis akiwa na mgombea Uwakilishi Bw. Mihayo N'hunga wakifuatilia kwa karibu mchakato wa kampeni hizo tawi la CCM mwera.



Diwani wa Wadi ya Mwera anayetetea nafasi yake katika uchaguzi mkuu mwaka huu Bi ShanI Omary Mbena akielezea mafanikio ya utekelezaji wa CCM na matarajio ya utekelezaji katika miaka mitano ijayo.





Baadhi ya wananchi wa jimbo la mwera waliojitokeza kusikiliza na kuwaunga mkono wagombea wa CCM katika uchaguzi mkuu. Kwa makini wakimsikiliza Mihayo N'hunga akielezea namna maendeleo ya kiuchumi na kwa vijana yatakavyo fikiwa. 


Baadhi ya wananchi wa jimbo la mwera waliojitokeza kusikiliza na kuwaunga mkono wagombea wa CCM katika uchaguzi mkuu. Kwa makini wakimsikiliza Mihayo N'hunga akielezea namna maendeleo ya kiuchumi na kwa vijana yatakavyo fikiwa

Saturday, September 26, 2015

VIONGOZI CHADEMA KUHAMIA CCM KILA KUKICHA

WAFUASI NA WANACHAMA WA CHADEMA MKOANI KAGERA KUAMUA HUHAMIA CCM NA KUHAKIKISHA KUMPA USHINDI JOHN P. MAGUFULI










Sunday, September 20, 2015

MIHAYO N'HUNGA AANZA KUNADI SERA BAADA YA KUZINDUA RASMI KAMPENI ZAKE KUWANIA UWAKILISHI



Chama Cha Mapinduzi (CCM) jimbo la Mwera kisiwani Unguja (Zanzibar) kimezindua rasmi kampeni zake ngazi ya jimbo kwa wagombea ngazi za Ubunge, Udiwani na Uwakilishi, ambapo umati mkubwa wa wanachama jimboni hapo walijitokeza ili kusikiliza sera za wagombea hao.
Mgombea Uwakilishi kupitia CCM jimboni hapo Bw. Mihayo N'hunga ambaye katika uzinduzi huo wa kampeni jimboni hapo ambaye ameongozana na makada mbalimbali wakiwemo Mgombea Ubunge wa jimbo hilo Bw. Makame Khamis, Diwani wa wadi ya Mwera Bi Sham ambaye pia ni mgombea wa nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu kupitia CCM.
Mwenye kiti wa Jumuiya ya wazazi ya CCM mkoa wa Mbeya Bi Fatuma Kasenga  ndiyo alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo ya uzinduzi wa kampeni hizo ambapo katika hotuba yake amehimiza kwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kuendelea kuwa wavumilivu licha ya propaganda na siasa za maji taka kutoka kwa wapinzani wao kisiasa. Akihutubia maelfu ya waliojitokeza katika uzinduzi huo, Bi Fatma Kasanga amesema, "Ndugu wana CCM, mwaka huu uchaguzi unaonekana kuwa na hamasa kubwa na wapinzani wanatumia propaganda, matusi na kejeli; lakini ndugu zangu tuwe wavumilivu sana na siasa zao za majitaka". Mgeni rasmi pia baada ya kuwatambulisha aliwanadi na kuwaombea kura wagombea wa CCM jimboni hapo na kuwataka washirikiane kuhakikisha CCM inapata ushindi mkubwa wa pamoja ili waweze kupata fursa nzuri kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo la Mwera.Naye mgombea Uwakilishi Bw. Mihayo N'hunga amesisitiza kuhakikisha kuleta maendeleo ya kiuchumi hasa kwa vijana ambao wengi wao ndio nguvu kazi kwa maendeleo ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla. Ameeleza kuwa atashirikiana vyema na m-bunge pamoja na madiwani kuwapigania vijana kwa kengo la kuwakwamua kiuchumi akiamini kwamba vijana ndio rika kubwa linalogusa kila familia na akasisitiza kwamba kumkwamua kijana ni kuijenga Zanzibar na Tanzania nzima.Akijibu hoja zinazoenezwa na wapinzani wake Bw. Mihayo amesema kwamba wanaodai kuwa yeye ni mdogo na hawezi kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo, je wao waliwatendea nini wananchi hao enzi za ujana wao. Mihayo amesikika akisema " Kuna wanao sema kuwa eti mimi ni mdogo, waulizeni wakati wao wakiwa na umri kama wangu, waliwatendea nini wanajimbo na wananchi".Alimalizia hotuba yake kwa kuwahakikishia wanachama wa chama hicho cha CCM kuwa waondoe shaka kwani safu nzima ya wagombea wa CCM jimboni hapo ni vijana wachapa kazi tu na kwamba wapo tayari kusimamia vyema ilani ya chama cha Mapinduzi kwani imesheheni mahitaji yote ya msingi. 

Kuelekea uchaguzi mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika October 25 wa uchagua viongozi wa ngazi za Rais, Ubunge, Uwakilishi (Zanzibar) na Udiwani, kwa jimbo la mwera Chama cha Mapinduzi (CCM) kinawakilishwa na wagombea mahiri ambao ni Bw. Makame Khamis (Ubunge), Bw. Mihayo N'hunga (Uwakilishi), na madiwani wawili ambao ni Bi Shani O. Mbena (Wadi ya Mwera) na Bw. Suleiman Abbas (Wadi ya Kianga). Kampeni hizo zilizinduliwa rasmi siku ya Ijumaa tarehe 18/09/2015 katika viwanja vya Misufini na kufuatiwa na mkutano wa hadhara kwa ajili hiyo uliofanyika Regeza Mwendo katika viwanja vya afisi za wilaya ya Magharibi nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

              Bw. Mihayo N'hunga akiwa kwenye picha ya pamoja na Bi Khadija Mussa Bi Amina muda mfupi kabla ya mkutano wa hadhara
 


Friday, September 11, 2015

"NI SAWA TUNATAKA MABADILIKO: JE NI YA MAGUFULI AU LOWASSA??" FUATILIA ALICHOANDIKA KIJANA HUMPHREY POLEPOLE KATIKA MTANDAO WA KIJAMII



NI SAWA TUNATAKA MABADILIKO:
 JE NI YA MAGUFULI AU LOWASSA??


Wagombea Urais wa CCM, Dr. John Magufuli na mwenzake wa CHADEMA Ndg Edward Lowassa wanakubaliana jambo moja kubwa: Haja ya kuwa na mabadiliko katika nchi yetu. Wagombea wote wameahidi kila mmoja kuwa iwapo atashinda ataleta mabadiliko. Tulinganishe sasa na kupima aina ya mabadiliko ambayo yanaweza kutokea iwapo mmojawapo atachaguliwa kuwa Rais wa nchi yetu.
Kulingana na historia ya utendaji wake katika wizara alizokabidhiwa na ahadi anazotoa mgombea wa CCM, Dr. John Magufuli, chini ya Urais wake inaonekana utawala wa sheria na nidhamu ya kazi kwa watumishi wa umma itatamalaki. Magufuli anajulikana zaidi kwa Watanzania kuwa ni mtu anayesimamia sheria hata pale zinapogusa maslahi ya wakubwa zake. Watanzania watakumbuka jinsi Magufuli alivyoweza kurudisha magari yaliyokuwa yameporwa kinyemela na vigogo wa serikali enzi za utawala wa Benjamin Mkapa.
Kwa upande wa Ndg. Edward Lowasa, iwapo atachaguliwa kuwa Rais, kuna uwezekano mkubwa kukawa na utawala unaotegemea hisia za Rais na ‘marafiki’ zake badala ya utawala wa sheria. Utendaji wake wa nyuma unaonyesha wazi kuwa Lowassa kama kiongozi ni mtu anayeamini matashi yake binafsi bila kuzingatia utawala wa sheria. Watanzania watakumbuka kuwa March 2006, akiwa waziri mkuu, Lowassa alimfukuza kazi mhandisi wa Manispaa ya Temeke bila kumpa nafasi ya kujitetea na tena mbele ya waandishi wa habari na kundi la wananchi waliokuwepo katika tukio la kuporomoka jengo la Chang’ombe Village.
Hivi karibuni, wakati anazindua kampeni zake, Lowassa alitoa ahadi kuwa ikiwa atashinda atamuchia huru Nguza Viking, maarufu kama Babu Seya aliyefungwa maisha jela kwa kwa kosa la kubaka na kulawiti watoto katika hukumu iliyotolewa na mahakama ya hakimu mkazi kisutu mwaka 2004. Kesi hiyo ilipelekwa katika mahakama ya rufaa mwaka 2010 na Mahakama ilikubaliana na uamuzi wa mahakama ya chini. Tena, mwaka 2013, jopo la majaji wa mahakama ya rufaa watatu likijumuisha Jaji Nathalia Kimaro, Mbarouk Mbarouk na Salum Msati walifanya mapitio ya mahakama hiyo na kuwaona wafungwa hao kuwa wana hatia.
Ikumbukwe kuwa sheria za Tanzania zinamyima Rais mamlaka ya kusamehe watu waliofungwa kwa makosa ya kubaka na kulawiti. Kwa kutamka kuwa atawachia wazi wafungwa hao,bila ya kusema chochote juu ya wale watoto waliolawitiwa na kubakwa na haja ya kufuata utawala wa sheria nchini ni dhahiri kuwa katika utawala wa Lowassa utawala wa sheria utawekwa kando na matashi ya watawala ndio yatakuwa yanaongoza nchi. Hili linadhibitishwa na ahadi nyingine ya Lowassa kuwa akiwa Rais, watuhumiwa wa kesi za ugaidi waliokamatwa huko Zanzibar wataachiwa huru kwa amri ya Rais. Ikumbukwe kuwa kwa sasa dunia iko kwenye vita dhidi ya ugaidi na ugaidi ni hatari kubwa na thahiri kwa maisha ya wananchi na mali zao.
Wagombea wote wameahidi kupambana na ufisadi na rushwa iwapo watachaguliwa kushika nafasi ya Urais. Magufuli ameahidi wazi kuwa ataleta mabadiliko katika vita dhidi ya rushwa na ufisadi kwa kuanzisha mahakama maalum ya kushughulikia masuala hayo. Kuna uwezekano mkubwa kuwa rushwa itaweza kudhibitiwa katika utawala wake ukizingatia kuwa katika harakati zake zote hakuungwa mkono na genge la mafisadi kama ilivyozoeleka kwa siasa za CCM tangu mwaka 2005 ilipotekwa na genge la wanamtandao.
Hali hii itamfanya aweze kutawala bila kuwa na deni la kulipa fadhila kwa mtu yeyote. Uzoefu wa siku za karibuni unaonyesha kuwa rushwa na ufisadi mkubwa unasababishwa na kujaza ‘marafiki’ katika nafasi muhimu za maamuzi. Kujaza marafiki hasa waliokufadhili kwenye harakati za uchaguzi kunafanya mifumo ya uwajibkaji katika nchi iwe na ganzi ya kufanya kazi dhidi ya marafiki hao.
Kwa upande wake Lowassa hajaeleza atafanya nini bayana katika kupambana na rushwa zaidi ya kusema atashughulikia rushwa. Kama ambavyo ilibainishwa na waziri mkuu mstaafu na mpambe wa Lowassa katika harakati za Urais, Fredrick Sumaye, katika viwanja vya jangwani, Lowassa ndiye mwasisi wa ‘mtandao’ uliomwingiza Rais Kikwete madarakani mwaka 2005. Kundi hili lilimjumisha pia Rostam Azizi na Laurence Masha ambao leo hii ndio pia ndio wanaongoza mikakati ya Lowassa. Rushwa katika mikataba ya aina mbalimbali na hata ukwapuaji wa fedha za umma kupitia maskandali mbalimbali kama EPA, Richmond na Dowans ulifanyika kama njia ya kulipa deni la fadhila wakati wa uchaguzi. Kama tulivyogusia hapo juu, ni vigumu kuchukua hatua dhidi ya marafiki na maswahiba.
Baada ya CCM kujikomboa kutoka katika makucha ya wanamtandao kwa kuwaondoa wagombea wa kundi hili akiwemo Lowassa kwenye kinyang’anyiro cha kugombea Urais kupitia chama hicho, kundi hilo limeweza ‘kuiteka nyara’ CHADEMA na kupitia kwake vyama vikuu vya upinzani kupitia UKAWA. Lowassa amesema waziwazi kuwa fedha anazogawa kwa wananchi mbalimbali zinatokana na ‘marafiki’ zake. Kwa hiyo, kama atachaguliwa, utawala wa Lowassa utaendeleza utawala wa wanamtandao, na watanzania watarajie kushamiri kwa ufisadi nchini kwa sababu tulizoeleza hapo juu.
Watanzania watakumbuka kuwa kile kinachoonekana kuwa ni ushabiki wa kupindukia kwa Lowassa hauna tofauti na ushbiki uliokuwepo mwaka 2005 kwa Kikwete. Hii inatokana na ukweli kuwa kundi linaloratibu na kuongoza kampeni za Lowassa ni lilile lililofanya kazi hiyo mwaka 2005. Tayari, kuna taarifa zinazosema kuwa wanamtandao wameshagawana nafasi muhimu za uongozi na mikataba katika maeneo manono kama bandari, madini na vitalu vya gesi na mafuta iwapo watafanikiwa kuiteka dola kupitia uchaguzi.
Magufuli ameahidi kuwa ataleta mabadiliko katika utendaji wa watumishi wa umma kwa kuweka mifumo imara ya uwajibikaji. Watu walio karibu na Magufuli wanasema kuwa Magufuli ameahidi kuwa akiwa Rais atawekeana mikataba ya utendaji kazi (Perfomance contracts) na mawaziri wake ambapo kila waziri ataingia kama yeye binafsi na akishindwa kufikia malengo atawajibishwa kwa kuondolewa madarakani. Magufuli ameahidi pia kuwa mafisadi watakaotiwa hatiani watafilisiwa mali zao.
Kwa upande wake Lowassa amesema kuwa akiingia madarakani atabadilisha mfumo wote wa nchi. Hii ina maana kuwa Lowassa akiwa Rais, taasisi za utawala kama vile Polisi, Jeshi, Utumishi wa Umma na vyombo vingine vitafumuliwa na kuundwa upya na kuwekwa watu wapya. Muhimu hapa ni kukubaliana kuwa siyo rahisi kwa jambo hilo kufanyika kwa kuwa kama ilivyo duniani kote yeyote atakaye shinda atalazimika kufanya kazi na vyombo hivyo. Mabadiliko yeyote ya utendaji wa vyombo hivyo vitategemea na hulka, tabia na haiba ya Rais. Hakika duniani kote mabadiliko katika nchi huletwa kwa vyombo hivyo kufanya kazi zao ipasavyo kutokana na uongozi na usimamizi dhabiti wa mkuu wa nchi.
Hitimisho
Haya ni baadhi ya mabadiliko yanaweza kutokea iwapo mmoja wa wagombea wetu watachaguliwa katika nafasi ya Urais. Mabadiliko haya yanaonyesha wazi kuwa uchaguzi ni muhimu sana kwa mustakabali wetu kama mtu mmoja mmoja na kama Taifa. Kwa sababu hiyo, ushabiki na uungwaji mkono wa wagombea lazima uzingatie faida na hasara zake kwa nchi na kwetu binafsi. Ni wakati wa kuwahoji na kuwatathimini wagombea wetu ili siku ya upigaji kura tisije tukafanya kosa litakalotuathiri sisi na vizazi vyetu. Tathmini hiyo ni muhimu kwa kujua kuwa utendaji kazi wa Rais huakisi na kuathiri utendaji kazi wa serikali na taasisi zote zilizo chini yake. Yaani Rais akiwa fisadi serikali na vyombo vyote chini yake vitakuwa vya kifisadi. La, Rais akiwa mwadilifu na mchapakazi na serikali yake itakuwa vivyo hivyo.
TUJADILIANE KWA HOJA NA SABABU.

Friday, August 28, 2015

SAMIA SULUHU ATANGAZA NEEMA KWA WAKAZI WA MKOA WA ARUSHA


Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa tiketi ya CCM akihutubia Jimbo la Arumeru.Baadhi ya wananchi na viongozi wa wafugaji wa kimasai wakifuatili kutano
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa tiketi ya CCM akihutubia Jimbo la Arumeru.Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa tiketi ya CCM akihutubia Jimbo la Arumeru.
Baadhi ya wanachama wa CCM wakimkabidhi zawadi katika mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu.Anjela Kairuki mmoja wa wajumbe wa kamati ya kampeni ya taifa akizungumza katika mkutano wa mgombea mwenza.Agrey Mwanri akizungumza na wapiga kura wake.Burudani kwa wananchi na mgeni rasmi katika mkutano wa hadhara moshi Mjini.Agrey Mwanri (kushoto) akifuraiya jambo na Bi. Ummy Mwalimu (kulia) kwenye mkutano wa B, Samia Sulu

Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa tiketi ya CCM akihutubia jimbo la Hai.
Baadhi ya wanachama na wapenzi wa CCM wakiwa katika mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Arusha Mjini.

Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa tiketi ya CCM akihutubia jimbo la Hai.
Baadhi ya wanachama na wapenzi wa CCM wakiwa katika mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Arusha Mjini.

Baadhi ya wanachama na wapenzi wa CCM wakiwa katika mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Arusha Mjini.

Burudani kwa wananchi na mgeni rasmi katika mkutano wa hadhara moshi Mjini. 
Na Joachim Mushi, Arusha
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kikifanikiwa kushinda Uchaguzi Mkuu wa Oktoba kitahakikisha mgambo wa halmashauri ya jiji hawawasumbui kwa kamatakamata za wafanyabiashara ndogondogo ambao wengi wao ni akinamama pamoja na vijana. Kauli hiyo imetolewa leo na mgombea mwenza nafasi ya urais tiketi ya CCM, Bi. Samia Suluhu alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara katika mkutano uliofanyika uwanja wa Kilombero Jimbo la Arusha Mjini na kuhudhuriwa na umati wa wanaCCM na wananchi wengine.
 
 Akinadi ilani ya CCM alisema chama hicho kimeandaa utaratibu mzuri wa fursa kwa akinamama na vijana wanaofanya biashara ndogondogo hivyo itakuwa ni marufuku kwa mgambo wa jiji kukamata biashara za akinamama na vijana wanaojitafutia ridhiki mjini. “…Iwapo CCM itafanikiwa kuingia mjini naomba wale mgambo ambao uishi kwa kutegemea kukamata kamata bidhaa za akinamama watafute kazi nyingine ya kufanyanya…hatutaki mgambo wa kufanya kazi hizo ni marufuku,
 
” alisema mgombea huyo mwenza wa CCM, Samia Suluhu. Alisema Ilani ya CCM imepanga kujenga viwanda vya kuchakata madini ili kuhakikisha vijana wanapata ajira na kuweza kukuza vipato vyao, na kufufua viwanda vilivyosimama kikiwemo cha ‘General Tyre’ ikiwa ni mpango wa kumaliza tatizo la ajira kwa vijana. Aidha alisema mpango mwingine ambao upo kwenye ilani ya CCM ni kushughulikia tatizo la mikataba ya ajira ya madereva wa magari madogo na makubwa, “..
 
.Tukifanikiwa kuingia Ikulu kazi ya kwanza tutakayoipa Wizara ya ajira ni kuhakikisha inafanya kazi ya kushughulikia mikataba ya ajira kwa madereva wa magari madogo na makubwa,” alisema Bi. Suluhu. Aliongeza Serikali ya CCM itaunda ufuko wa maji kuakikisha huduma za maji zinakuwa za uhakika kwani Mkoa wa Arusha unashughuli nyingi na idadi ya watu inakuwa kila uchao. Serikali ya CCM imepanga kushughulikia suala la rushwa na vitendo vya ufisadi, uzembe ili kuhakikisha kasi ya maendeleo inaongezeka. Awali kabla ya mkutano wa Arusha Bi. Suluhu alifanya mikutano katika majimbo ya Hai, Siha na Arumeru yaliyopo mikoa ya Kilimanjaro kabla ya kuingia Mkoani Arusha. Akiwa katika majimbo hayo mgombea aliinadi ilani ya CCM pamoja na kuwanadi wagombea ubunge na madiwani wa CCM wa maeneo hayo. Ambapo alisema Serikali ya CCM imepanga kuboresha huduma za afya, elimu, uwezeshaji wa vijana na akinamama ikiwa ni pamoja na kutenga shilingi milioni 50 kwa kila kijiji kwa ajili ya kuwainua akinamama na vijana. 

Wednesday, August 26, 2015

MJUE MGOMBEA UTAKAYEMPIGIA KURA october 25.


Kumekua na utamaduni ulijenga imani kwa jamii kuamini kwamba kura ni siri kwa mpigaji tu wa kura hizo. Lakini hali imekua tofauti kwa makada na hata mashabiki na wafuasi wa vyama mbali mbali hapa nchini.
Hili limedhihirika hasa pale makada na mashabiki vyama fulani vya siasa kuonesha misimamo yao waziwazi juu ya kuunga mkono chama ama mgombea wa chama fulani na kujivunia kua ushindi wa chama chake utasababiswa na yeye kuelekeza kura yake kwa chama hicho.
Kumekua na mijadala ya wazi tena wakati mwingine kwa mabishano, wakitaniana kuwa "mwaka huu nyie lazima muwanguke", ama "nyie mtaisoma namba" lakini pia kumekua na kujiamini na hata kutambiana kwamba "mgombea wetu jembe" ilimuradi tu kila mwanachama kudhihirisha kuwa kurake isiwe siri na ijulikane mapema misimamo ya yao ni kwa mgombea/ chama fulani.
Baadhi wa watumiaji wa mitandao ya kijamii wamefikia hata kuwafuta urafiki marafiki zao wa muda mrefu mitandaoni, kwa sababu tu ya kukithiri kuweka post/mada ama picha za kudhihirisha msimamo wao kisiasa.
Lakini kwa upande mwingine, kughihirisha kuunga mkono chama/mgombea fulani kumeonekana kuongeza uwazi katika nyanja hii ya siasa kwani hata wahombea ama chama huongeza nguvu kwa wanachama wake tu kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi, kuanzia kujiandikisha, kushiriki kwenye mikutano ya chama na kampeni na hata kuomba ridhaa ya uongozi.
Kuoelekea uchaguzi mkuu October 25 mwaka huu, mchuano mkali umejitokeza hasa kwa wagombea kiti cha Rais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM dhidi ya mpinzani wake wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.
Uchaguzi mkuu Tanzania hufanyika kila baada ya miaka mitano ambapo viongozi katika nafasi za Urais, Ubunge, Uwakilishi (Zanzibar) na Udiwani huchaguliwa kwa kuzingatia mfumo wa kidemokrasia za vyamba vingi.







Monday, August 24, 2015

MAGUFULI AWEKA HISTORIA RUVUMA KATIKA KAMPENI ZA URAIS TANZANIA

PICHA ZA MATUKIO MBALI MBALI ZA MGOMBEA URAIS WA CCM WAKATI WA KAMPENI ZA CHAMA HICHO MJINI RUVUMA