Tuesday, October 20, 2015

MPANGO WA SIRI WA CHADEMA KUHUJUMU C.U.F; NCCR MAGEUZI; NA NLD





Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA katika mchakato wa UKAWA kimekua kikiratibu mipango kabambe ambayo imekua ni kinyume na makubaliano baina ya chama hicho na vyama vingine vya C.U.F, NCCR Mageuzi na NLD.
Licha ya kwamba vyama hivyo vingine havina wawakilishi wenye nguvu kufanya maamuzi ya chama, mfano Chama cha Wananchi C.U.F bara hakina Mwenyekini wala Makamu Mwenyekiti, wakati NLD mwenyekiti wake ambaye sasa ni marehemu, alikua pia mgombea ubunge lakini CHADEMA walifanya hila wakamkataa na kumnyang'anya jimbi na kuliweka mikononi mwao.
Mapema baada ya kuanza kwa kampeni za uchaguzi nchini, CHADEMA walitoa waraka wa siri wenye azimio la kutokuwaunga mkono wagombea wa vyama hivyo washirika na kufanya mpango wa kuchukua majimbo yao, jambo ambalo wamelifanikisha katika semu kubwa.
Njama za kuwarubuni waendesha bodaboda na makundi kadhaa ya vijana ni moja ya mipango mikubwa ambayo wanaamini wanaweza kufanikisha kupigania matakwa yao kisiasa. 

No comments:

Post a Comment