Monday, September 14, 2015

"NIMEJIPANGA VYEMA KWA UZINDUZI WA KAMPENI" MIHAYO N'HUNGA

 MIHAYO N'HUNGA "NIMEJIPANGA VYEMA KWA UZINDUZI WA KAMPENI"

Mgombea UWAKILISHI jimbo la mwera huko visiwani Zanzibar Nd. Mihayo N'hunga (pichani) amesema tayari amekamilisha sehemu kubwa ya maandalizi ya kampeni zake tayari kukabiliana na wapinzani katika uchaguzi mkuu jimboni hapo. Akizungumza kwa njia ya simu muda mfupi baada ya kumalizika kwa mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za CCM mjini Zanzibar Mihayo amesema kwamba kulingana na hatua iliyofikiwa kwa ajili ya mchakato mzima wa kampeni mpaka kufikia uchaguzi anawahakikishia wanajimbo na wanachama wote kwa ujumla kuwa ushindi kwa CCM haukwepeki.  "Kwa kweli namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa namna maandalizi ya mchakato mzima wa kampeni kukamilika na mpaka sasa napenda kuwahakikishia wana CCM wote nchini, hususan wanajimbo la Mwera kuwa tutashinda Uchaguzi tena kwa kishindo. Pamoja na changamoto kadhaa za kifedha na nyingine nyingi lakini namshukuru sana Mungu kwani nafarijika na hamasa na muamko wa wanajimbo kwani nimekuwa napokea salamu nyingi kuungwa mkono hata na ngome kuu za wapinzani jimboni kwangu, hili limenipa nguvu sana".





No comments:

Post a Comment