
HABARI HATIMAYE NAPE AFUNGUKA KUHUSU MCHAKATO UNAOENDELEA KWENYE UTEUZI WA URAIS CCM, DODOMA
Hatimaye Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama cha Mapinduzi (CCM)Nape Nnauye ameongea na waandishi wa habari asubuhi ya hii ya saa 3 kuhusu mchakato wa kuteua mgombea wa Urais kupitia chama cha CCM unaoendelea Dodoma.
Nape Nnauye amesema kwamba siku ya juzi na jana hakikufanyika kikao chochote kama ilivyokuwa imepangwa hapo awali ila vikao vitatu muhimu vitafanyika siku ya leo.
"Leo hii saa 4 asubuhi kinaanza Kikao cha kamati ya maadili na usalama ya chama ambacho kitaenda hadi saa 7 au 8 mchana, halafu kitafuata Kikao cha kamati kuu ya CCM (CC) ambacho kitafanyika leo kuanzia saa 8 mchana hadi saa 11 au 12 jioni na kupitisha majina matano ya wagombea, halafu baada ya watu kula futari kitaanza kikao cha halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) ambapo watapitisha majina ya wagombea watatu." Amesema Nape Nnauye
Nape amesema kuwa usiku wa leo yatapatikana majina ya wagombea watatu baada ya kikao cha halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) kukaa na kesho siku ya jumamosi ratiba ya mkutano mkuu wa CCM iko pale pale ili kumpitisha mgombea atakayegombea Urais kupitia chama cha CCM
Amesema kuwa sababu mbili za kuchelewa vikao hivyo ni kuwa Mwenyekiti wa CCM Dr. Jakaya Kikwete alikuwa amebanwa na shughuli nyingi za chama na serikali na pia kutokana na mchakato wa mwaka huu kuwa mkubwa sana walikuwa kwanza na vikao mbalimbali vya mashauriano na wadau wa ndani ya chama na nje ya chama ,pia ushauri toka serikalini.
Nape amewataka watu wanaotoa habari za uvumi kwenye mitandao ya jamii waache mara moja maana habari hizo zinachanganya watu na habari kamili itatolewa na CCM
No comments:
Post a Comment