Friday, July 17, 2015

MIHAYO N'HUNGA AGOMBEA UWAKILISHI JIMBO LA MWERA



MIHAYO N’HUNGA ACHUKUA FOMU YA UWAKILISHI CCM JIMBO LA MWERA KUMRITHI MH. SHAWANA BUHETI 

Leo imekua siku ya kipekee kwa kijana anayechipukia kwa kasi ya juu kisiasa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi CCM mkoa wa mjini Magharibi visiwani Zanzibar na mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM, baada ya kutangaza nia na kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa na chama hicho kupeperusha bendera ya CCM kugombea Uwakilishi jimbo la Mwera katika uchaguzi mkuu mwishoni mwaka huu. Tukio hilo lilitokea leo katika ofisi za CCM wilaya ya magaharibi zilizopo Regeza mwendo mjini Unguja. 
Aliyekuwa Mwakilishi Mh. Shawana Buheti Hassan alitangaza kutogombea tena nafasi hiyo.

Akizungumzia sababu hasa zinazompelekea kugombea wadifa huo, bw. Mihayo amesema kwamba, pamoja na kushauriwa na makundi ya vijana na hata wazee wenye busara kumtaka afanye hivyo, bali pia amejitathmini na kubaini kuwa yeye ndio chaguo bora hasa kwa wanachi wanaoishi jimboni hapo. "Kwa kweli nimekua nikipokea ushauri toka kwa wanachama wenye rika tofauti pamoja na vijana na wazee wenye busara, na pia mimi mwenyewe nimeona kwamba nina ari ya kujituma katika mabo ninayofanya na napenda kuona mafanikio ya kazi zangu". "Huu ni wakati ambao jamii inahitaji watu wanaojituma katika kuutumikia umma na sio wanaopenda kuvaa koti la uongozi. Kwa sababu mimi bado ni kijana ambaye bado nina uchu na ari kubwa ya maendeleo, ninataka niwe ndio sababu ya maendeleo katika mazingira yangu".

Historia yake Kielimu
Mihayo N'hunga ni mzaliwa wa Mwera katika familia ya aliyekua Mbunge wa mda mrefu mahali hapo Mh. Juma S. N'hunga ambaye aliamua kustaafu mwaka 2010. Mihayo alianza elimu ya msingi katika Skuli ya Regezamwendo na baadae kuhamia Shule ya msingi K/Ndege ambapo alipalizia elimu ya msingi. Alijiunga na shule ya secondary ya Lomwe iliyoko Usangi wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro kabla ya kupata uhamisho na kumalizia elimu ya secondary shule ya St. Mathew, na baadaye kujiunga na elimu ya secondary ya juu (High School) katika shule ya Ubungo Islamic iliyopo Dar es Salaam. Kwa sasa Mihayo ni msomi wa chuo kikuu fani ya Sheria Zanzibar University.
Hata hivyo, muda mwingi akiwa masomoni, Mihayo ametumia muda wake mwingi kuwatumikia wanafunzi wenziwe katika ngazi mbalimbali


 Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Mjini Magharibi visiwani Zanzibar Bw. Mihayo N'hunga akionesha Fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea Uwakilishi ya chama chake CCM katika uchaguzi mkuu utakaofanyika October 25 mwaka huu. Tukio hilo lilifanyika katika ofisi ya CCM wilaya leo.

 Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Mjini Magharibi visiwani Zanzibar Bw. Mihayo N'hunga akimkabidhi katibu wa CCM wa wilaya fedha taslim ikiwa ni malipo ya Uchukuaji fomu ya kutangaza nia ili kupata ridhaa na kuteuliwa kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu ujao mwaka huu.


Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Mjini Magharibi visiwani Zanzibar Bw. Mihayo N'hunga akikabidhiwa fomu za kutangaza nia ili kupata ridhaa na kuteuliwa kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu ujao mwaka huu. Kulia ni katibu wa CCM wilaya ya Magharibi.

Wiki iliyopita Mihayo N'hunga aliungana na makada wengine wa CCM kuhudhuria mkutano mkuu wa chama hicho mjini Dodoma katika mchakato wa kumpata mgombea Urais wa Muungano na pia wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi, ambapo Dr. Ali Mohamed Shein (Zanzibar) aliteuliwa bila kupingwa, na Dr. John Pombe Magufuli kupata ushindi wa kishindo. Mh. Samia Suluhu aliteuliwa kuwa mgombea mwenza urais wa Muungano.

Katika hafla hiyo Mihayo alipata fursa pia ya kukutana faragha na makanda wenye nguvu ndani ya CCM na pia alikutana na baadhi ya watia nia (Wagombea) katika mchakato huo wa chama kama vile Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Kimataifa ambaye pia ni mmoja wa watiania aliyefika hadi top five Mh. Bernard Membe; Mwingulu, Januari, Asha-Rose Migiro, Ridhwani Kikwete, Makongoro Nyerere, na wengine wengi.

 Mihayo N'hunga akiwa na Mh. Bernard Membe

 Mihayo N'hunga akiwa na Ridhwani Kikwete

 Mihayo N'hunga akiwa na Mjumbe wa NEC Bi. Lulu Msham

 Mihayo N'hunga akiwa na Mh. Asha-Rose Migiro 

 Mihayo N'hunga akiwa na January Makamba na Naibu waziri wa Mawasiliano

Mihayo N'hunga akiwa na Mh. Mwingulu Nchemba

  








No comments:

Post a Comment