
Alasiri hii halmashauri kuu ya
chama hicho inafanya kikao chake kupata majina matatu, halafu baadae leo jioni
mkutano mkuu wa chama hicho unatarajiwa kukaa kupigia kura jina moja kati ya
hayo matatu.
Yule atakayeibuka mshindi kati ya
watatu hao ndiye atakaye kuwa mgombea urais wa chama hicho katika uchaguzi mkuu
ujao unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu
Hata hivyo kutangazwa kwa majina
matano na kamati kuu ya halmashauri kuu ya taifa (CC-NEC) ya chama hicho jana
usiku, kuliibua mgawanyiko miongoni mwa wajumbe wa kamati hiyo, ambapo watatu
wa wajumbe 32 wa kamati hiyo waliibuka wazi na kupinga uteuzi wa majina hayo
mbele ya vyombo vya habari

Watanzania kumjua ni nani atakayekuwa mgombea urais kwa ticket ya CCM katika uchaguzi mkuu ujao
Wajumbe waliopinga uteuzi huo ni Dk. Emmanuel Nchimbi,
Sophia Simba na Adam Kimbisa
Wajumbe hao walidai kuwa kanuni
za utendaji katika vikao vilivyotangulia kamati kuu zimekiukwa na kufafanua
kwamba kamati hiyo ilipokea majina matano kutoka kamati ya maadili na usala,
badala ya kupewa majina yote ya walioomba kuteuliwa, halafu yenyewe ndiyo
ichambue majina matano.
“Kanuni zinasema Kamati Kuu
itapokea majina ya waombaji wote na ikishafanya uchambuzi wa kila muombaji,
yakiwemo maoni ya kamati ya usalama na maadili, ndiyo huchagua majina matano
yanayofikishwa mbele ya Halmashauri Kuu,” alihoji Dk. Nchimbi

Mpasuko
huu unaonekana kuwa mwanzo wa kutimia kwa utabiri wa wachambuzi mbalimbali
ambao walionya mchakato huu unahatarisha uhai wa chama kikongwe nchini Tanzania
Majina matano yaliyopitishwa na Kamati Kuu ni Bernard
Membe (Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dk. John Magufuli
(Waziri wa Ujenzi) Dk. Asha-Rose Migiro (Waziri wa Katiba na Sheria) January
Makamba (Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia) na Balozi Amina
Salum Ali (Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Tume ya Umoja wa Afrika
kwenye Umoja wa Mataifa, Marekani)
Kufikia Jumapili, tarehe 12. Julai, Watanzania
watakuwa wamejua ni nani atakayekuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM kwa
uchaguzi mkuu ujao
No comments:
Post a Comment