Saturday, June 20, 2015

KINANA: TAIFA LATAKIWA KUJENGWA KWA MISINGI YA KUJITEGEMEA




Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara Katoro.



Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Katoro mkoani Geita ambapo aliwaambia wananchi hao mwekezaji mzuri nchi wa kwanza ni mwananchi mwenyewe, pia alizungumzia sheria ambazo  nyingi zinazowakadamiza wananchi,zinapoteza nguvu kazi,zinawanyima haki wachimbaji wadogo zapaswa kufutwa.



Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Katoro waliojitokeza kwa wingi ,Katika mkutano huo Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi aliwaambia wakazi hao vyama vingi vya siasa vimeshindwa kuendelea kutokana na kukosa sera,kushindwa kusimamia mambo pamoja na kuwa na viongozi wasiokubali mabadiliko na kung'ang'ania madaraka.




Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitoa somo la siasa kwa wakazi wa Kata ya Katoro.



Mbunge wa Jimbo la Busanda Mhe.Mh Lolensia Bukwimba akihutubia wakazi wa Katoro kwenye mkutano wa hadhara ambao mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana



Wananchi wa kata ya Katoro wakishangilia ujio wa Kinana 


No comments:

Post a Comment