
Dk. John Pombe Joseph Magufuli, alizaliwa Oktoba 29, 1959 wilayani Chato – wakati huo ikiwa Mkoa wa Kagera (sasa Mkoa wa Geita).
Ana Shahada ya Uzamivu ya Kemia (2006 – 2009) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mwaka 1991 – 1994, alisoma Shahada ya Uzamili (Kemia) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na baadaye Chuo Kikuu cha Salfordnchini Uingereza.
Mwaka 1985 – 1988, alisoma Shahada ya Kwanzaya Elimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akichukua masomo ya Kemia na Hisabati.
Mwaka 1981 – 1982, alisoma diploma katika Chuo cha Mkwawa akichukua masomo ya Kemia na Hisabati.
Mwaka 1979 – 1981, alipata elimu ya juu ya sekondari katika Shule ya Sekondari Mkwawa, Iringa.
Mwaka 1977 – 1978, alisoma elimu ya sekondari katika Shule ya Sekondari Lake, Mwanza.
Mwaka 1975 – 1977, alisoma Shule ya Msingi Katoke, Biharamulo mkoani Kagera.
Mwaka 1967 – 1974, alisoma Shule ya Msingi, Chato.
Mafunzo
Machi 1984 – Juni 1984 alihudhuria mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Mpwapwa mkoani Dodoma.
Januari 1984 – Machi 1984 alikuwa JKT Makuyuni, Arusha.
Julai 1983 – Desemba 1983 alikuwa JKT Makutupora, Dodoma.
Uzoefu wa kazi
Mwaka 2010 – hadi sasa: Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Chato.
Mwaka 2008 – 2010: Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Samaki; Mbunge wa Biharamulo Mashariki (Chato).
Mwaka 2005 – 2008: Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; na Mbunge wa Biharamulo Mashariki (Chato)
Mwaka 2000 – 2005: Waziri wa Ujenzi, na Mbunge wa Biharamulo Mashariki.
Mwaka 1995 – 2000: Naibu Waziri wa Ujenzi; na Mbunge wa Biharamulo Mashariki.
Mwaka 1989 – 1995: Mkemia Chama cha Ushirika cha Nyanza Cooperative Union (Ltd.), Mwanza.
Mwaka 1982 – 1983: Mwalimu Shule ya Sekondari Sengerema (akifundisha masomo ya Kemia na Hisabati).
Dk. Magufuli amepata tuzo mbalimbali za ndani na nje ya nchi.
Ameshiriki na kuongoza mikutano mingi ya kitaifa na kimataifa.
Ameandika vitabu na majarida mbalimbali. Ameoa na ana watoto kadhaa.
Salutation | Hon. | Member picture![]() | |
First Name: | Dr. John | ||
Middle Name: | Pombe Joseph | ||
Last Name: | Magufuli | ||
Member Type: | Elected Member | ||
Constituent: | Chato | ||
Political Party: | Chama Cha Mapinduzi | ||
Office Location: | P.O. Box 9144, Dar es Salaam | ||
Office Phone: | +255 713 322 272/+255 754 292 580 | Office Fax: | + 255 22 2124505 |
Office E-mail: | jmagufuli@parliament.go.tz | ||
Member Status: | Active | ||
Date of Birth | 29 October 1959 |
Chato Primary School | CPEE | 1967 | 1984 | Primary School |
Katoke Seminary Biharamulo, Kagera | CSEE | 1975 | 1977 | Secondary School |
Mkwawa High School | ACSEE | 1979 | 1981 | Secondary School |
Lake Secondary School ¿ Mwanza | CSEE | 1977 | 1978 | Secondary School |
Mkwawa College of Education | Diploma in Education (Sc.) Chem., Maths&Edu. | 1981 | 1982 | Diploma |
University of Dar es Salaam | B.Sc Ed. (Hons) Chem.&Maths | 1985 | 1988 | Bachelor |
Universities of Dar es Salaam, TZ &Salford -U.K. | MSc. (Chem) | 1991 | 1994 | Masters Degree |
University of Dar es Salaam. | PhD (Chem) | 2006 | 2009 | PhD |
UN-HABITAT | Co-chair World Urban Forum (III) | 2006 | To Date |
Ministry of Lands and Human Settlements | Minister | 2005 | 2/8/2008 |
World Road Congress (PIARC) | 1st Delegate | 2000 | 2005 |
Mtwara Development Corridor | Member | 2000 | 2005 |
Ministry of Works | Minister | 2000 | 2005 |
Ministry of Works | Deputy Minister | 1995 | 2000 |
Tanzania Chemical Society | Member | 1993 | Todate |
Nyanza Co-operative Union(NCU) Ltd.- Mwanza. | Industrial Chemist | 1989 | 1995 |
Sengerema Secondary School | Teacher(Chemistry and Mathematics) | 1982 | 1983 |
Ministry of Livestock and Fisheries Development | Minister | 13/02/2008 | To Date |
Ministry/Political Party/Location | Position | From | To |
---|---|---|---|
Chama Cha Mapinduzi - CCM( Biharamulo East) | Member of Parliament of Tanzania | 1995 | Todate |
Chama Cha Mapinduzi - CCM
CHAMA Cha Mapinduzi
(CCM) kimempitisha Dk. John Pombe Magufuli kuwa mgombea urais kupitia chama
hicho.
Kwa
mujibu wa taarifa kutoka ndani ya kikao hicho, Dk. Magufuli amepita kwa kura
hizo kutokana na nguvu yake dhidi ya wagombea wengine.
“Hakukuwa na namna hapa kwa kuwa, wajumbe wanaamini katika mazingira haya magumu ya upinzani Dk. Magufuli anaaminika na kukubalika nje kuliko hawa wengine,” anasema mtoa taarifa wetu ambaye toka ndani ya kamati maalum na kuongeza kwamba; “Baada ya kutemwa Membe (Bernard Membe) kwenye NEC kila mjumbe ambaye alikuwa upande wa Lowassa (Edward Lowassa) alipumua jambo lililomrahisishia Magufuli.” Mkutano huo umehairishwa mpaka saa nne asubuhi, ambapo ndiyo muda ambao Dk. Magufuli ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Mashariki na Waziri wa Ujenzi atatangazwa rasmi kuwa mgombea wa Urais kupitia chama hicho. Awali ndani ya ukumbi wa mkutano, kulidawa kuwepo kwa mpango wa wafuasi wa Lowassa kutaka kumpitisha Balozi Amina ili chama hicho kipate changamoto katika ‘kumuuza’ kwa wananchi ikiwa ni kulipiza kisasi kwa kukatwa mtu wao (Lowassa). Katika Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya chama hicho, majina yaliyopitishwa yalikiwa ni Migiro, Magufuli, Balozi Amina, Membe na January Makamba. |
No comments:
Post a Comment